Orodha ya Hadithi

Hakika ninachokiogopea zaidi juu yenu ni shirki ndogo" Wakasema: Ni ipi shirki ndogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni riyaa (kujionyesha)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Niliyokukatazeni basi yaepukeni, na yale niliyokuamrisheni basi yaleteni katika hayo kadiri muwezavyo, na hakika waliangamia wale waliokuwa kabla yenu, kwa kukithiri maswali yao, na kuhitilafiana kwao na Manabii wao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mtu mwenye tabia nzuri mno kuliko watu wote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Basi tabia ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ilikuwa ni Qur'ani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kukimpendeza sana kuanzia kulia katika kuvaa kwake viatu, na kuchana kwake nywele, na kujisafisha kwake, na katika mambo yake yote.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Sikumuona Mtume -Rehema Amani ziwe juu yake- katu akipitiliza kucheka mpaka kionekane Kilimi ndani ya mdomo wake, bali alikuwa akitabasamu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Nilihifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- rakaa kumi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hivi nikuhadithieni hadithi kuhusu Dajali ambayo hajawahi kuhadithia Nabii yeyote watu wake! Hakika yeye ni chongo, na hakika yeye atakuja akiwa pamoja na mfano wa pepo na moto, anayoisema kuwa ni pepo huo ndio moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu, Ole wao waarabu kutokana na shari iliyokaribia, imefunguliwa leo katika ngome ya Ya-ajuju na Ma-juju mfano wa hiki, na akachora duara kwa vidole vyake viwili, kidole gumba na kile kinachofuata, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Hivi tunaweza kuangamizwa hali miongoni mwetu kuna wema? Akasema: Ndiyo, pindi uchafu utakapokithiri.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume Rehema na Amani zimfikie na haya (aibu) nyingi kuliko msichana bikra akiwa chumbani kwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Muabuduni Mwenyezi Mungu peke yake msimshirikishe yeye na chochote, na acheni wanayosema baba zenu, na anatuamrisha swala na ukweli
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yakwamba Nabii -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa safarini, akaswali swala ya ishaa ya mwisho, akasoma katika moja ya rakaa mbili kwa sura ya wattin wazzaitun, sijawahi kumsikia yeyote mwenye sauti nzuri au kisomo kizuri zaidi yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yakwamba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alikuwa anapo swali anatanua kati ya mikono yake mpaka unaonekana weupe wa kwapa lake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakuna kwa baba yako matatizo baada ya leo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapopiga chafya anaweka mkono wake au nguo yake juu ya kinywa chake, na anapunguza sauti yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yalikuwa maneno ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ni maneno ya wazi anayaelewa kila mwenye kuyasikia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Laiti nisingeliogopea uzito kwa umma wangu; ningeliwaamrisha kupiga mswaki kila wakati wa swala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Nitampa bendera kesho mtu ambaye anampenda Allah na Mtume wake,na anapendwa na Allah na Mtume wake,kupitia yeye Allah ataleta ushindi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akiitembelea msikiti wa Qubaa kwa kipando na pia kwa miguu, anaswali ndani yake rakaa mbili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hivi hukujua kuwa uislamu hufuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, na kuwa kuhama kunafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake, nakuwa Hija inafuta madhambi yaliyokuwa kabla yake?
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Nilikuwa nikioga mimi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika chombo kimoja sisi wote tukiwa na janaba, na alikuwa akiniamrisha najifunga kikoi (kishida), ananigusa na mimi nikiwa katika hedhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Aliingia Abdur Rahmani bin Abiibakari As swiddiq -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- na mimi nikiwa nimemuegemeza kifuani kwangu, na Abdur Rahmani -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- akiwa na mswaki mbichi akisukutua nao, akauelekezea Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- macho yake-.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alifariki Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- hali yakuwa hakuna chochote nyumbani kwake anachoweza kukila mwenye ini (uhai) ila kiasi kidogo cha ngano kilichokuwa katika ubao wangu (wa kuhifadhia chakula), nikala mpaka kikakaa muda mrefu, nilipokipima kikamalizika
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume wa Allah -rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu kuliko watu wote, na alikuwa mkarimu zaidi anapokuwa katika mwezi wa Ramadhani pindi anapokutana na Jibrili
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakuna yeyote atakayenisalimia isipokuwa Mwenyezi Mungu hunirudishia roho yangu ili nimjibu salam
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Walikuwa wana wa Israeli wakiongozwa na Manabii, kila anapokufa nabii anafuatiwa na nabii mwingine, na hakika hakuna nabii baada yangu, na watafuata Makhalifa (viongozi) baada yangu, na watakithiri
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
"Wana nini watu waliosema kadhaa wa kadhaa? lakini mimi ninaswali na ninalala na ninafunga na ninakula, na ninaoa wanawake; atakayeuchukia muongozo wangu basi hayuko nami
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakuwahi kupewa hiyari Mtume rehema na amani ziwe juu yake baina ya mambo mawili hata siku moja isipokuwa atachukua jepesi lake, madamu si dhambi, ikiwa itakuwa ni dhambi, basi hujiwekanalo mbali kuliko watu wote
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu