عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا قَالَ:
أُنْزِلَ عَلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ ابْنُ أَرْبَعِينَ، فَمَكَثَ بِمَكَّةَ ثَلَاثَ عَشْرَةَ سَنَةً، ثُمَّ أُمِرَ بِالْهِجْرَةِ، فَهَاجَرَ إِلَى الْمَدِينَةِ، فَمَكَثَ بِهَا عَشْرَ سِنِينَ، ثُمَّ تُوُفِّيَ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3851]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yao- amesema:
Uliteremshwa Wahyi kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka arobaini, akakaa Makkah miaka kumi na tatu, kisha akaamrishwa kuhama, hivyo akahama kwenda Madina, akakaa Madina miaka kumi, kisha akafariki Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3851]
Anaeleza Bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: kuwa Wahyi uliteremshwa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na akatumwa akiwa na umri wa miaka arobaini, basi akakaa Makkah miaka kumi na tatu baada ya kuteremshiwa wahyi, kisha akaamrishwa kuhama kwenda Madina na akakaa huko miaka kumi, kisha akafariki -Rehema na amani ziwe juu yake- akiwa na umri wa miaka sitini na tatu.