Aina: Akida- Itikadi- .
+ -

عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال:
بَيْنَمَا نَحْنُ عِنْدَ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ذَاتَ يَوْمٍ إِذْ طَلَعَ عَلَيْنَا رَجُلٌ شَدِيدُ بَيَاضِ الثِّيَابِ، شَدِيدُ سَوَادِ الشَّعَرِ، لَا يُرَى عَلَيْهِ أَثَرُ السَّفَرِ، وَلَا يَعْرِفُهُ مِنَّا أَحَدٌ، حَتَّى جَلَسَ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَسْنَدَ رُكْبَتَيْهِ إِلَى رُكْبَتَيْهِ، وَوَضَعَ كَفَّيْهِ عَلَى فَخِذَيْهِ، وَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ، أَخْبِرْنِي عَنِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْإِسْلَامُ أَنْ تَشْهَدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا رَسُولُ اللهِ، وَتُقِيمَ الصَّلَاةَ، وَتُؤْتِيَ الزَّكَاةَ، وَتَصُومَ رَمَضَانَ، وَتَحُجَّ الْبَيْتَ إِنِ اسْتَطَعْتَ إِلَيْهِ سَبِيلًا» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَعَجِبْنَا لَهُ، يَسْأَلُهُ وَيُصَدِّقُهُ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِيمَانِ، قَالَ: «أَنْ تُؤْمِنَ بِاللهِ، وَمَلَائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ، وَرُسُلِهِ، وَالْيَوْمِ الْآخِرِ، وَتُؤْمِنَ بِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ» قَالَ: صَدَقْتَ، قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ الْإِحْسَانِ، قَالَ: «أَنْ تَعْبُدَ اللهَ كَأَنَّكَ تَرَاهُ، فَإِنْ لَمْ تَكُنْ تَرَاهُ فَإِنَّهُ يَرَاكَ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنِ السَّاعَةِ، قَالَ: «مَا الْمَسْؤُولُ عَنْهَا بِأَعْلَمَ مِنَ السَّائِلِ» قَالَ: فَأَخْبِرْنِي عَنْ أَمَارَتِهَا، قَالَ: «أَنْ تَلِدَ الْأَمَةُ رَبَّتَهَا، وَأَنْ تَرَى الْحُفَاةَ الْعُرَاةَ الْعَالَةَ رِعَاءَ الشَّاءِ يَتَطَاوَلُونَ فِي الْبُنْيَانِ» قَالَ: ثُمَّ انْطَلَقَ، فَلَبِثْتُ مَلِيًّا ثُمَّ قَالَ لِي: «يَا عُمَرُ، أَتَدْرِي مَنِ السَّائِلُ؟» قُلْتُ: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «فَإِنَّهُ جِبْرِيلُ، أَتَاكُمْ يُعَلِّمُكُمْ دِينَكُمْ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 8]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Siku moja tukiwa tumekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ghafla akatokea mtu mwenye nguo nyeupe mno, mwenye nywele nyeusi mno, haonekani kuwa na athari yoyote ya safari, na hakuna yeyote amjuaye miongoni mwetu, akaja mpaka akakaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakunja magoti yake kwa kuyaunganisha na magoti yake mtume (Mithili ya tahiyatu) Na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake, na akasema: Ewe Muhammadi, nieleze kuhusu Uislamu, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Uislamu ni ushuhudie kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na usimamishe sala, na utoe zake, na ufunge Ramadhani, na uhiji katika nyumba tukufu ikiwa utapata uwezo wa kuifikia" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), Anasema: Tukamshangaa: Anamuuliza na anamsadikisha! Akasema: Nieleze kuhusu imani. Akasema: "Nikuwa, umuamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na vitabu vyake, na Mitume wake, na siku ya mwisho, na uamini Kadari kheri yake na shari yake" Akasema: Sadakta! (Umesema kweli), akasema: Nieleza kuhusu Ihisani, akasema: "Ni umuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba unamuona, na ikiwa wewe humuoni basi yeye anakuona" Akasema: Nieleze kuhusu Kiyama, akasema: "Muulizwaji si mjuzi sana kama muulizaji" Akasema: Hebu nieleze kuhusu alama zake, akasema: "Ni mjakazi kuzaa bosi wake, na ukiwaona watembea peku, watembea uchi, tena masikini wachunga mbuzi, wakishindana kujenga majengo marefu." (Omar) Akasema: Kisha akaondoka, nikakaa muda mrefu kidogo, kisha Mtume akasema kuniambia: "Ewe Omari, hivi unamjua ni nani muulizaji?" Nikasema: Allah na Mtume wake ndio wajuzi zaidi, akasema: "Huyo ni Jibrili alikuja kukufundisheni dini yenu."

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 8]

Ufafanuzi

Anaeleza Omari bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Jibrili -Amani iwe juu yake- alijitokeza kwa Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- kwa sura ya mtu asiyejulikana, na miongoni mwa sifa zake nikuwa, nguo zake ni nyeupe mno, na nywele zake ni nyeusi mno, haonekani kuwa na athari za safari ikiwemo kuonyesha uchovu, vumbi, na nywele kutimka, na nguo kuchafuka, na hakuna yeyote amjuaye katika wote waliopo, nao wakiwa wamekaa kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, akakaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkao wa mwanafunzi, akamuuliza kuhusu Uislamu, akamjibu kwa nguzo hizi ambazo zimeambatana na kukiri shahada mbili, na kudumu na sala tano, na kutimiza zaka kwa wastahiki wake, na kufunga mwezi wa Ramadhani, na kutekeleza faradhi ya Hija kwa mwenye uwezo.
Muulizaji akasema: Sadakta!, Masahaba wakashangaa kwa swali lake la kuonyesha kuwa hajui kitu kwa muonekano wake, kisha anamsadikisha!.
Kisha akamuuliza kuhusu imani, akamjibu kwa nguzo hizi sita zilizokusanya kuamini uwepo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa zake, na kumpwekesha kwa vitendo vyake kama kuumba, na kumpwekesha kwa ibada, nakuwa Malaika aliowaumba Allah kwa nuru ni waja waliotukuzwa hawamuasi Mwenyezi Mungu Mtukufu, na amri yake ndio wanayoifanyia kazi, na kuamini vitabu vilivyoteremshwa kwa Mitume kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kama Qur'ani na Taurati na Injili na vinginevyo, na kuwaamini Mitume wenye kumfikishia Mwenyezi Mungu dini yake, miongoni mwao ni Nuhu na Ibrahim, na Mussa, na Issa, na wa mwisho wao ni Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yao wote- na wengineo katika Manabii na Mitume, na kuamini siku ya mwisho, na yanaingia hapa maisha baada ya kifo ikiwemo kaburi na maisha ya barzakh (Akhera), na kuamini kuwa Mwenyezi Mungu amekadiria mambo kulingana na ujuzi wake uliotangulia na hekima zake zikapelekea hivyo, na kuyaandika kwake, na matashi yake kwa mambo hayo, na kutokea kwake kwa namna aliyoikadiria Mwenyezi Mungu, na kuviumba kwake. Kisha akamuuliza kuhusu Ihisani, akamueleza kuwa Ihisani ni amuabudu Mwenyezi Mungu kana kwamba anamuona, ikiwa hatoweza kufikia daraja hili basi amuabudu Allah kana kwamba Allah anamshuhudia, daraja bora zaidi kushuhudiwa, na ndio ya juu zaidi, na ya pili ni daraja ya kuchunga (Kuleta hisia kua unamuona mbele yako).
Kisha akamuuliza Kiyama ni lini? Akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa elimu ya Kiyama ni katika elimu alizobaki nazo Mwenyezi Mungu ujuzi wake, hawezi kuijua yeyote katika viumbe, si muulizaji wala muulizwaji.
Kisha akamuuliza kuhusu alama za Kiyama? Akabainisha kuwa miongoni mwa alama zake ni kukithiri kwa wajakazi (Masuria) na watoto wao, au ni wingi wa watoto kutowatii mama zao, kiasi cha kuishi nao kama watumwa wao, nakuwa wachunga mbuzi na masikini watakunjuliwa dunia katika zama za mwisho, na watafaharishana katika kuremba majengo na kuyarefusha.
Kisha akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa muulizaji ni Jibril alikuja kuwafundisha Masahaba dini tukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kwani alikuwa akikaa na wanafunzi wake, nao wakikaa kwake.
  2. Sheria ya kuwa mpole kwa muulizaji na kumsogeza karibu, ili aweze kuuliza bila wasi wasi wala uoga.
  3. Kuwa na adabu na mwalimu kama alivyofanya Jibril -Amani iwe juu yake-, kiasi kwamba alikaa mbele ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkao wa adabu ili ajifunze toka kwake.
  4. Nguzo za Uislamu ni tano, na misingi ya Imani ni sita.
  5. Linapokutana neno Uislamu na Imani Uislamu hutafirisiwa kwa mambo ya dhahiri (yenye kuonekana) na Imani kwa mambo yasiyoonekana.
  6. Kumebainishwa kuwa dini ina daraja tofauti, daraja la kwanza: Ni Uislamu, la pili: Imani, na la tatu: Ihisani, na ndio la juu zaidi kuliko yote.
  7. Kimsingi muulizaji hua si mjuzi, na ujinga ndio msukumo wa kuuliza, ndio maana Masahaba walishangaa kuuliza kwake na kusadikisha kwake.
  8. Kuanza na la muhimu zaidi kisha linalofuata; Kwa sababu kumeanzwa na shahada mbili katika tafsiri ya Uislamu, na kumeanzwa na kumuamini Mwenyezi Mungu katika tafsiri ya imani.
  9. Inafaa mjuzi kuwauliza wajuzi mambo anayoyafahamu kwa lengo la kuwafundisha wengine.
  10. Elimu ya Kiyama ni katika elimu alizobaki nazo Allah.
Aina tofauti