Aina: Akida- Itikadi- .
+ -

عن أبي ذر رضي الله عنه:
عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِيمَا رَوَى عَنِ اللهِ تَبَارَكَ وَتَعَالَى أَنَّهُ قَالَ: «يَا عِبَادِي إِنِّي حَرَّمْتُ الظُّلْمَ عَلَى نَفْسِي، وَجَعَلْتُهُ بَيْنَكُمْ مُحَرَّمًا، فَلَا تَظَالَمُوا، يَا عِبَادِي كُلُّكُمْ ضَالٌّ إِلَّا مَنْ هَدَيْتُهُ، فَاسْتَهْدُونِي أَهْدِكُمْ، يَا عِبَادِي كُلُّكُمْ جَائِعٌ إِلَّا مَنْ أَطْعَمْتُهُ، فَاسْتَطْعِمُونِي أُطْعِمْكُمْ، يَا عِبَادِي كُلُّكُمْ عَارٍ إِلَّا مَنْ كَسَوْتُهُ، فَاسْتَكْسُونِي أَكْسُكُمْ، يَا عِبَادِي إِنَّكُمْ تُخْطِئُونَ بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَأَنَا أَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا فَاسْتَغْفِرُونِي أَغْفِرْ لَكُمْ، يَا عِبَادِي إِنَّكُمْ لَنْ تَبْلُغُوا ضَرِّي فَتَضُرُّونِي، وَلَنْ تَبْلُغُوا نَفْعِي فَتَنْفَعُونِي، يَا عِبَادِي لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ كَانُوا عَلَى أَتْقَى قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ مِنْكُمْ مَا زَادَ ذَلِكَ فِي مُلْكِي شَيْئًا، يَا عِبَادِي لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ كَانُوا عَلَى أَفْجَرِ قَلْبِ رَجُلٍ وَاحِدٍ مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِنْ مُلْكِي شَيْئًا، يَا عِبَادِي لَوْ أَنَّ أَوَّلَكُمْ وَآخِرَكُمْ وَإِنْسَكُمْ وَجِنَّكُمْ قَامُوا فِي صَعِيدٍ وَاحِدٍ فَسَأَلُونِي فَأَعْطَيْتُ كُلَّ إِنْسَانٍ مَسْأَلَتَهُ مَا نَقَصَ ذَلِكَ مِمَّا عِنْدِي إِلَّا كَمَا يَنْقُصُ الْمِخْيَطُ إِذَا أُدْخِلَ الْبَحْرَ، يَا عِبَادِي إِنَّمَا هِيَ أَعْمَالُكُمْ أُحْصِيهَا لَكُمْ ثُمَّ أُوَفِّيكُمْ إِيَّاهَا، فَمَنْ وَجَدَ خَيْرًا فَلْيَحْمَدِ اللهَ، وَمَنْ وَجَدَ غَيْرَ ذَلِكَ فَلَا يَلُومَنَّ إِلَّا نَفْسَهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2577]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Dharri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-katika yale aliyoyapokea kutoka kwa Mola wake Mtukufu hakika Yeye amesema: "Enyi waja wangu hakika Mimi nimeharamisha dhulma juu ya Nafsi yangu na nikaifanya kuwa ni haramu baina yenu, basi msidhulumiane, enyi waja wangu nyote ni wapotevu isipokuwa yule niliye muongoza, basi niombeni uongofu nami nitakuongozeni, enyi waja wangu nyote ni wenye njaa isipokuwa yule niliye mlisha, basi niombeni chakula nami nitakulisheni, enyi waja wangu nyote mpo uchi isipokuwa yule niliye mvisha, basi niombeni kuvaa nami nitakuvisheni, enyi waja wangu hakika nyinyi mnakosea usiku na mchana na mimi ninasamehe madhambi yote, basi niombeni msamaha nami nitakusameheni, enyi waja wangu hamtafikia kufanya madhara ili mnidhuru wala hamtafanya mambo yenye manufaa ili mninufaishe, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakawa na ucha Mungu wa mtu mmoja hilo lisinge niongezea chochote katika Ufalme wangu chochote, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wakijikusanya wote wakafanya uovu wa mtu mmoja hilo lisinge punguza chochote katika Ufalme wangu, enyi waja wangu laiti wa mwanzo wenu na wa mwisho wenu binadamu na majini wangejikusanya katika uwanja mmoja wakaniomba nikampa kila mtu alicho kiomba hilo lisinge punguza chochote katika Ufalame wangu isipokuwa ni kama sindano inavyo punguza maji pindi inapo ingizwa baharini, enyi waja wangu si vinginevyo bali hakika matendo yenu yote nina wahifadhieni kisha nitawapa malipo yenu, mwenye kupata kheri amshukuru Mwenyezi Mungu, na atakayepata kinyume na hayo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake."

Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa amejiharamishia dhulma juu ya Nafsi yake, na akaifanya dhulma kuwa haramu baina ya waja wake, hivyo mtu asimdhulumu yeyote, Nakuwa viumbe wote wamepotea katika njia ya haki isipokuwa kwa uongofu wa Mwenyezi Mungu na taufiki yake, na atakayemuomba Mwenyezi Mungu uongofu basi atamuafikisha na atamuongoza, Nakuwa viumbe wote ni mafukara kwa Mwenyezi Mungu, wote ni wahitaji kwake katika haja zao zote, na atakayemuomba Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamtimizia haja zake na atamtosheleza, Nakuwa wao hutenda dhambi usiku na mchana, na Mwenyezi Mungu Mtukufu husitiri na husamehe pale mja anapomuomba msamaha, Nakuwa wao hawawezi kumdhuru Mwenyezi Mungu au kumnufaisha kwa chochote, Nakuwa wao lau kama wangelikuwa katika uchamungu wa moyo wa mtu mmoja, uchamungu wao usingeongeza chochote katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu, Na lau kama wangelikuwa katika uovu wa moyo wa mtu mmoja, uovu wao usingepunguza chochote katika Ufalme wake; kwa sababu wao ni madhaifu na mafakiri na ni wahitaji kwake kwa kila hali na kwa nyakati zote na mahala popote, na yeye ni mkwasi na utakasifu ni wake. Na lau kama wangelisimama mahala pamoja binadamu wao na majini wao, wa mwanzo wao na wa mwisho wao, wakimuomba Mwenyezi Mungu, akampa kila mmoja miongoni mwao ombi lake, hilo lisingepunguza chochote katika vile vilivyoko kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa ni kama mfano wa sindano inapoingizwa Baharini kisha ikatolewa, Bahari kamwe haipungukiwi na kitu, na hii ni kwa sababu ya ukamilifu wa utajiri wake Mtukufu.
Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anayahifadhi matendo ya waja na kisha anawatunzia, kisha anawatimizia malipo siku ya Kiyama, atakayekuta malipo ya matendo yake yakiwa ni kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumuafikisha kwake katika kumtii, na atakayekuta malipo ya matendo yake ni kinyume na hivyo basi asilaumu ila nafsi yake yenye kuamrisha maovu iliyompelekea katika hasara.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية القيرقيزية النيبالية اليوروبا الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية الكينياروندا الرومانية المجرية التشيكية المالاجاشية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hadithi hii ni miongoni mwa yale anayoyapokea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutoka kwa Mola wake, na inaitwa hadithil Qudsiy au Hadithi Ilahiy, nayo ni ile ambayo matamshi yake na maana yake inatoka kwa Mwenyezi Mungu, isipokuwa haina daraja kama ya Qur'ani ambayo inasifika nayo ukilinganisha na vingine, kama kufanya ibada kupitia kisomo chake na usafi wake, na kutoa kwake changamoto kwa wasomi na mengine mengi.
  2. Kinachotokea kwa waja kwanzia elimu au kuongoka, ni kwa muongozo wa Mwenyezi Mungu na elimu yake.
  3. Haimpati mja kheri yoyote isipokuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na haimpati shari isipokuwa inatoka katika nafsi yake na matamanio yake.
  4. Atakayefanya vizuri basi ni kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu, na malipo yake ni fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo anastahiki sifa, na atakayefanya uovu basi asilaumu ila nafsi yake.