عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِنَّ اللهَ لَا يَنْظُرُ إِلَى صُوَرِكُمْ وَأَمْوَالِكُمْ، وَلَكِنْ يَنْظُرُ إِلَى قُلُوبِكُمْ وَأَعْمَالِكُمْ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2564]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2564]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hatazami sura za waja na miili yao, je ni nzuri au mbaya? Je ni mikubwa au midogo? Ina afya au maradhi? Na wala hatazami katika mali zao, je ni nyingi au kidogo? Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka hawaadhibu waja wake wala hawahesabu kwa mambo haya na kutofautiana kwao, lakini anatazama katika nyoyo zao na yale yaliyomo ndani miongoni mwa uchamungu na yakini, na ukweli na ikhlaswi, au ni lengo la kujionyesha au kutaka kusikika, na anatazama katika matendo yao upande wa usahihi wake au kuharibika kwake; Hapo atatoa thawabu na malipo kwa hayo.