Orodha ya Hadithi

Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Wakristo, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa misikiti- Anatahadharisha waliyoyafanya- na lau isingekuwa kauli hiyo basi lingedhihirishwa kaburi lake, (Angezikwa nje) ispokuwa alihofia kufanywa kuwa msikiti.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mimi nimejitosheleza na washirika juu ya kushirikishwa; atakayefanya jambo lolote akamshirikisha pamoja nami mwingine nitamuacha na shirki yake au (na mshirika wake).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika mimi najiepusha kwa Mwenyezi Mungu kuwa kwangu kati yenu na rafiki wa ndani, kwani Mwenyezi Mungu amenifanya mimi kuwa kipenzi wa ndani kama alivyomfanya Ibrahim kuwa kipenzi wa ndani, na lau kama ningejifanyia kipenzi wa ndani katika umma wangu basi ningemfanya Abuubakari kuwa kipenzi wa ndani.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapata wivu, na wivu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuyafanya mtu yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu kwake yeye.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
"Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyochupa mipaka manaswara kwa mwana wa Mariam, bila shaka hakika mimi ni mja wake, basi semeni; mja wa Mwenyezi Mungu na mjumbe wake"
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni nani atakayefurahika zaidi kwa utetezi wako? Akasema: Atakayesema Laa ilaaha illa llaahu (Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu) kwa nia safi toka moyoni mwake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, Atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayekufa naye akiomba kinyume na Mwenyezi Mungu mshirika, ataingia motoni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wameangamia wenye kujilazimisha -Alilisema hilo mara tatu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu ameandika mema na mabaya kisha akalibainisha hilo, atakayepania kufanya jema kisha akawa hakulifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake jema kamili, na akilipania na akalifanya analiandika Mwenyezi Mungu kwake kuwa ni mema kumi mpaka kufikia ziada ya mia saba mpaka ziada nyingi zaidi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu hatazami katika mili yenu wala katika sura zenu, lakini anaangalia katika nyoyo zenu na matendo yenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Enyi waja wangu, Hakika mimi nimeharamisha dhulma katika nafsi yangu na nimeifanya kati yetu kuwa ni haramu hivyo msidhulumiane, Enyi waja wangu, nyinyi wote mmepotea ila yule niliyemuongoza niombeni uongofu nikuongozeni
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimuuliza Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Ni dhambi ipi kubwa? Akasema: Ni kumuwekea Mwenyezi Mungu mshirika, na haliyakuwa yeye ndiye aliyekuumba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Je nikuagize katika yale aliyoniagiza kwayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake? Usiache picha yoyote ispokuwa umeifuta, wala kaburi lililonyanyuliwa ispokuwa umelisawazisha.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Madhambi makubwa kuliko yote: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kujiaminisha na adhabu za Mwenyezi Mungu, na kukata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu, Na kufa moyo katika huruma za Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba yeye alikuwa pamoja na Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake katika baadhi ya safari zake, akatuma mjumbe asibakishe katika shingo ya mnyama chochote kinachotundikwa ispokuwa kikatwe.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayesema: Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, na akayapinga yanayoabudiwa kinyume na Mwenyezi Mungu, ni haramu mali yake, na damu yake, na hesabu yake ni juu ya Mwenyezi Mungu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Wenye huruma huwahurumia Ar-Rahmani -Mwingi wa huruma-, wahurumieni watu wa ardhini atakuhurumieni aliyeko mbinguni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Malaika huteremka katika mawingu- wakalitaja jambo lililopitishwa mbinguni, basi shetani huiba kusikia, na akalisikia, kisha akaliteremsha kwa makuhani kisha wanaongopa pamoja na neno hilo uongo mia moja toka kwao wenyewe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna mja yeyote atakayeshuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammdi ni mja wake kwa kusadikisha kutoka moyoni mwake ispokuwa atamharamisha Mwenyezi Mungu kuingia motoni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Huteremka Mola wetu Aliyetakasika na kutukuka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho Anasema: Nani mwenye kuniita, nimjibu, nani mwenye kuniomba nimpe, nani mwenye kuniomba msamaha nimsamehe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiswali makaburini, wala msiyakalie makaburi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hao ni watu ambao anapokufa kwao mja mwema, au mtu mwema, wanajenga juu ya kaburi lake msikiti, na wanachora hapo mapicha, hao ni viumbe waovu mbele ya Mwenyezi Mungu.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Umejengwa uislamu kwa mambo matano
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni msije kuapa (kupitia) kwa baba zenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Msiseme: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu na matakwa ya fulani, lakini semeni: Ni matakwa ya Mwenyezi Mungu kisha akataka fulani
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
kuapa kwangu kwa jina la Mwenyezi Mungu kwa uongo napenda zaidi kuliko kuapa kwa jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu nikisema ukweli
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni nini kinachowaogopesha hawa? wanapatwa na ulaini (wanazikubali) katika aya zilizo wazi, na wanaangamia katika aya zinazotatiza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si chochote mbingu saba na ardhi saba katika kiganja cha Ar-Rahmaani -Mwingi wa rehema- isipokuwa ni kama punje ya ulezi katika mkono wa mmoja wenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Si chochote kursiy (Mahala anapoweka miguu Ar-Rahmani) katika Arshi isipokuwa ni kama bangili la chuma lililowekwa katika ardhi ya jangwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakuna kuambukizana maradhi, wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini. Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: Ni neno jema
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Fanyeni matendo na muwe na msimamo, na tambueni kuwa hatosalimika mmoja wenu kwasababu ya matendo yake, wakasema: Hata wewe Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?! Akasema: Hata mimi isipokuwa atakaponifunika mimi Mwenyezi Mungu kwa huruma zake na fadhila zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Amesema Mwenyezi Mungu -Mtukufu- mimi niko katika dhana ya mja wangu kwangu, na mimi niko pamoja naye pindi anaponikumbuka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hato msitiri mja mja mwenzie duniani isipokuwa atamsitiri Mwenyezi Mungu siku ya kiyama
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tulikuwa kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- watu tisa au nane au saba, akasema: Hivi hamumpi ahadi ya utiifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayepatwa na umasikini akaushusha kwa watu hautozibwa umasikini wake, na atakayeushusha kwa Mwenyezi Mungu, basi ni karibu zaidi Mwenyezi Mungu kumpa riziki ya haraka au ya baadaye
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika Mwenyezi Mungu ameniondolea mimi kwa umma wangu (madhambi ya) kukosea na kusahau, na yale waliyolazimishwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa