عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : "لا عدوى وَلَا طِيَرَةَ، وَيُعْجِبُنِي الفَأْلُ. قالوا: وما الفأل؟ قال: الكلمة الطيِّبة".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Hakuna kuambukizana maradhi wala kutuhumu mikosi kwa sababu ya ndege, na kinachonipendeza zaidi ni kujipa matumaini. Wakasema: Ni nini matumaini? Akasema: Ni neno jema".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Kwakuwa kheri na shari zote hukadiriwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, alikanusha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi hii swala la ugonjwa kuathiri wenyewe binafsi, na akakanusha uwepo wa athari za ndege, na akathibitisha swala la matumaini na akalipendezesha; na hii ni kwakuwa matumaini ni kumdhania vizuri Mwenyezi Mungu, Na ni kichocheo cha malengo katika kuhakikisha malengo yanatimia, kinyume na imani za mikosi na nuksi. Na katika sentensi hii kuna tofauti kati ya matumaini na mikosi kwa namna nyingi, Ya kwanza: 1- Matumaini huwa kwa mambo yanayofurahisha, na mikosi huwa haiwi ila kwa mambo yanayochukiza. 2- Matumaini ndani yake kuna dhana nzuri kwa Mwenyezi Mungu, na mikosi ndani yake kuna dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu, na mja kakatazwa kuwa na dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno
Kuonyesha Tarjama
Ziada