عن عمر بن الخطاب رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «لا تُطْروني كما أَطْرت النصارى ابنَ مريم؛ إنما أنا عبده، فقولوا: عبد الله ورسوله».
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na Amani zimfikie akisema: "Msichupe mipaka katika kunisifu kama walivyochupa mipaka manaswara kwa mwana wa Mariam, bila shaka hakika mimi ni mja wake, basi semeni; mja wa Mwenyezi Mungu na mjumbe wake"
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Nikuwa Mtume rehema na Amani zimfikie pupa yake juu ya kumpwekesha Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na kwakuuhofia umma wake juu ya shirki ambayo ziliangukia umma zilizotangulia, akautahadharisha na kuchupa mpaka kwake, na kupita kiasi katika kumsifu, mfano kama kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu- na kwa matendo yake maalumu kwake, kama walivyovuka mpaka manaswara kwa Isa kwa kumsifu kwa uungu na utoto wa Mwenyezi Mungu -Mtukufu- wakaangukia katika shirki kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakika wamekufuru wale waliosema Hakika Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Mariam, na alisema Masihi; 'Enyi wana wa Israeli, muabuduni Mwenyezi Mungu Mola wangu na Mola wenu, hakika yeyote mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia juu yake pepo, na makazi yake ni motoni, na madhalimu hawatokuwa na wakuwanusuru" kisha akasema: "Hakika mimi ni mja wake, basi semeni mja wake na Mtume wake" Yaani: Nisifuni kwa uja na utume kama alivyonisifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hilo, na wala msivuke mpaka kwangu wa utumwa mpaka katika nafasi ya uungu au ulezi kama walivyofanya wakristo, kwani haki ya Manabii ni utumwa na utume, ama uungu hiyo ni haki ya Mwenyezi Mungu peke yake, lakini pamoja na tahadhari hii tayari kuna watu wamekwisha tumbukia katika yale aliyoyatahadharisha Mtume rehema na Amani zimfikie, Chunga usiwe miongoni mwao.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kutahadhari na kuvuka mpaka na kupitiliza katika kusifu, na kuvuka kiwango, na kusifia kwa batili; kwasababu hilo linaweza kupelekea katika shirki, na kumshusha mja katika nafasi ya uungu, na kumsifu kwa sifa zake -Mtukufu-.
  2. Nikuwa ukafiri wa wakristo ulikuwa kwa kuvuka kwao mpaka kwa Masihi na watakatifu wa kiume na wa kike waliokuja baada yake, na kauli yao kwa Issa kuwa yeye ni mwana wa Mungu, mpaka likawapelekea hilo kupindisha vitabu vitakatifu; ili wavitumie kama hoja ya usahihi wa madai yao ya batili.