+ -

عن عائشة أم المؤمنين وعبد الله بن عباس رضي الله عنهما قالا:
لَمَّا نَزَلَ بِرَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طَفِقَ يَطْرَحُ خَمِيصَةً لَهُ عَلَى وَجْهِهِ، فَإِذَا اغْتَمَّ بِهَا كَشَفَهَا عَنْ وَجْهِهِ، فَقَالَ وَهُوَ كَذَلِكَ: «لَعْنَةُ اللَّهِ عَلَى اليَهُودِ وَالنَّصَارَى، اتَّخَذُوا قُبُورَ أَنْبِيَائِهِمْ مَسَاجِدَ» يُحَذِّرُ مَا صَنَعُوا.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 435]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha na Abdillah bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao wamesema:
Yalipomfika Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mauti akawa anaweka nguo yake juu ya uso wake, anapozidiwa kupumua anaifunua kutoka usoni kwake, na anasema naye akiwa katika hali hiyo: "Laana za Mwenyezi Mungu ziwe juu ya Mayahudi na Maswara, waliyafanya makaburi ya Manabii wao kuwa ni Misikiti" Akitahadharisha waliyoyafanya.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 435]

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha na bin Abbasi -Radhi za Allah ziwe juu yao- yakuwa kilimpofika kifo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alianza kuweka kipande cha kitambaa juu ya uso wake, akibanwa na pumzi kwa sababu ya kilevi cha kifo anakitoa usoni kwake, akasema akiwa katika hali hiyo mbaya: Mwenyezi Mungu amewalaani Mayahudi na Manaswara, na akawafukuza kutoka katika rehema yake; na hii ni kwa sababu wao walijenga Misikiti juu ya makaburi ya Manabii wao, laiti kama jambo hili lisingekuwa na hatari basi asingelieleza katika sehemu kama hii, kwa sababu hii ameukataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kufanana na kitendo hicho; kwa sababu ni katika vitendo vya Mayahudi na Manaswara, na ni kwa sababu ni njia inayopelekea katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kukatazwa kuyafanya makaburi ya Manabii na watu wema kuwa Misikiti inayoswaliwa kwaajili ya Mwenyezi Mungu, kwasababu hilo ni njia inayopelekea katika ushirikina.
  2. Kipaumbele kikubwa cha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuitilia umuhimu tauhidi na hofu yake juu ya kutukuzwa makaburi; kwa sababu hilo linapelekea katika ushirikina.
  3. Inafaa kuwalaani Mahayudi na Manaswara na atakayefanya mfano wa vitendo vyao ikiwemo kuyajengea makaburi na kuyafanya kuwa mahali pa ibada.
  4. Kujengea makaburi ni katika taratibu za Mayahudi na Manaswara, na katika hadithi hii kuna katazo la kujifananisha nao.
  5. Miongoni mwa kuyafanya makaburi kuwa misikiti ni kuswali hapo au kuswali kwa kuyaelekea, hata kama hapajajengwa msikiti.