عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ:
قِيلَ: يَا رَسُولَ اللهِ، مَنْ أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِكَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ؟ قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَقَدْ ظَنَنْتُ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ أَنْ لَا يَسْأَلَنِي عَنْ هَذَا الْحَدِيثِ أَحَدٌ أَوَّلُ مِنْكَ؛ لِمَا رَأَيْتُ مِنْ حِرْصِكَ عَلَى الْحَدِيثِ، أَسْعَدُ النَّاسِ بِشَفَاعَتِي يَوْمَ الْقِيَامَةِ، مَنْ قَالَ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ خَالِصًا مِنْ قَلْبِهِ أَوْ نَفْسِهِ»».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 99]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Palisemwa ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni mtu gani atakayepata furaha zaidi ya uombezi wako siku ya Kiyama? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Nilijua kuwa ewe Abuu Huraira hatoniuliza mwingine hadithi hii kabla yako, kwa kile nilichokiona kwako, pupa yako juu ya hadithi, Mtu atakayepata furaha zaidi ya uombezi wangu siku ya Kiyama, ni yule atakayesema Laa ilaaha illa llah (Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu), kwa kutakasa nia toka moyo mwake au nafsi yake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 99]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mtu mwenye furaha zaidi kuliko wote kwa uombezi wake siku ya Kiyama ni yule atakayesema: "Laa ilaaha illa llaah kwa kutakasa nia toka moyoni mwake" Yaani: Hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na asalimike na ushirikina na riyaa(kufanya mambo kwa kujionesha).