عن عبادة بن الصامت رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم "مَنْ شهِد أنْ لا إله إلا الله وحده لا شرِيك له وأنَّ محمَّدا عبده ورسُولُه، وأنَّ عِيسى عبدُ الله ورسُولُه وكَلِمَتُه أَلقَاها إِلى مريم ورُوُحٌ مِنه، والجنَّة حَقٌّ والنَّار حقٌّ، أَدْخَلَه الله الجنَّة على ما كان مِنَ العمَل".
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ubada bin swamit-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume rehema na Amani zimfikie: "Atakaye shuhudia kuwa hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mjumbe wake na ni mja wake, nakuwa Issa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na neno lake alilolipeleka kwa Mariam na ni roho toka kwake, na pepo ni kweli na moto ni kweli, Atamuingiza Mwenyezi Mungu peponi kulingana na yale aliyokuwa nayo katika matendo".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Inatueleza hadithi hii kuwa mwenye kutamka neno la Imani (Tauhiidi) na akajua maana yake na akayafanyia kazi malengo yake, na akashuhudia uja wa Muhammadi rehema na Amani zimfikie na ujumbe wake, na akakiri uja wa Issa na ujumbe wake, nakuwa yeye aliumbwa kwa neno "Kuwa" kutoka kwa Mariam, na akamuepusha mama yake na yale waliyomnasibishia maadui mayahudi, na akaitakidi kuthibiti kwa pepo kwa waumini na kuthibiti kwa moto kwa makafiri, na akafa katika imani hiyo ataingia peponi kulingana na yale yaliyokuwa katika matendo.