عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«مَنْ لَقِيَ اللهَ لَا يُشْرِكُ بِهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ لَقِيَهُ يُشْرِكُ بِهِ دَخَلَ النَّارَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 93]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri bin Abdillah -Radhi za Allah ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakayekutana na Mwenyezi Mungu akiwa hamshirikishi na chochote basi ataingia Peponi, na atakayekutana naye akimshirikisha ataingia Motoni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 93]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kufa hali yakuwa hamshirikishi Mwenyezi Mungu na chochote basi mafikio yake ni katika Pepo hata kama ataadhibiwa kwa baadhi ya madhambi yake, nakuwa atakayekufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote atabakizwa milele Motoni.