عن عبد الله بن عمرو بن العاص - رضي الله عنه- مرفوعاً: "مَن ردته الطِّيَرَة عن حاجته فقد أشرك، قالوا: فما كفارة ذلك؟ قال: أن تقول: اللهم لا خير إلا خيرك، ولا طَيْرَ إِلَّا طَيْرُكَ ولا إله غيرك".
[صحيح] - [رواه أحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillah bin Amri bin Aaswi- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Itakayemrudisha imani ya mkosi wa ndege akaacha shida yake basi atakuwa amefanya shirki, wakasema: Ni ipi kafara ya hilo? Akasema: ni useme: Ewe Mwenyezi Mungu hakuna kheri ila kheri yako, na hakuna ndege ispokuwa ndege wako, na hakuna Mola zaidi yako.
[Sahihi] - [Imepokelewa na Ahmad]
Anatueleza Mtume rehema na Amani zimfikie katika hadithi hii kuwa yeyote itakayemzuia mikosi kutoliendea alilolikusudia basi huyu atakuwa kaleta aina miongoni mwa aina za ushirikina, na walipomuuliza maswahaba juu ya kafara ya dhambi hili kubwa aliwaelekeza katika ibara hizi tukufu katika hadithi ambayo inakusanya kulielekeza jambo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu- na kukanusha uwezo kwa asiyekuwa yeye.