عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما مرفوعاً: "من حلف بغير الله قد كفر أو أشرك"
[صحيح] - [رواه الترمذي وأبو داود وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillahi bin Umar- Radhi za Allah ziwe juu yake- akisimulia kutoka kwa Mtume : " Mwenye kumuapia asiyekuwa Allah atakuwa kakufuru au kamshirikisha Allah".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy
Anatupa habari Mtume- Rehema na amani ziwe juu yake-katika hadithi hii, habari ambayo maana yake ni katazo: kwamba mwenye kukiapia chochote kinyume na Allah,miongoni mwa viumbe, basi atakuwa kakifanya kiumbe hicho alichokiapia kuwa ni mshirika wa Allah ,na atakuwa amekufuru, maana kukiapia kitu inamaana ya kukiadhimisha na kiuhakika utukufu wa kweli ni wa Allah pekee, hivyo asiapiwe asiyekuwa Allah,au sifa miongoni mwa sifa zake.