+ -

عَن عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنين رضي الله عنها زَوْجَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدَّثَتْهُ قَالَتْ:
جَاءَتْنِي امْرَأَةٌ مَعَهَا ابْنَتَانِ تَسْأَلُنِي، فَلَمْ تَجِدْ عِنْدِي غَيْرَ تَمْرَةٍ وَاحِدَةٍ، فَأَعْطَيْتُهَا فَقَسَمَتْهَا بَيْنَ ابْنَتَيْهَا، ثُمَّ قَامَتْ فَخَرَجَتْ، فَدَخَلَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَحَدَّثْتُهُ، فَقَالَ: «مَنْ يَلِي مِنْ هَذِهِ البَنَاتِ شَيْئًا، فَأَحْسَنَ إِلَيْهِنَّ، كُنَّ لَهُ سِتْرًا مِنَ النَّارِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5995]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alimsimulia akasema:
Alinijia mwanamke mmoja akiwa na watoto wake wawili akiniomba, nikawa sikupata ndani kwangu zaidi ya tende moja, nikampatia, akaigawanya baina ya watoto wake, kisha akanyanyuka akatoka, muda si mrefu, akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamsimulia kisa hicho, akasema: "Atakayesimamia chochote kwa watoto wa kike hawa, akawatendea wema, basi watakuwa ni kinga kwake kutokana na moto".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5995]

Ufafanuzi

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake, ya kwamba mwanamke mmoja alimjia akiwa na mabinti zake wawili akimuomba chochote kinacholiwa, Aisha akawa hakupata kwake zaidi ya tende moja, akampatia basi mwanamke yule akaigawanya tende hiyo baina ya watoto wake, na yeye hakula chochote, kisha akanyanyuka na akaondoka, punde akaingia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, Aisha akamsimulia kisa hicho, akasema: Atakayesimamia chochote katika malezi ya mabinti hawa, akawatendea wema na akawalisha na akawanywesha na akawavisha, na akawa na subira juu ya hilo, basi watakuwa ni sitara na kinga kwake dhidi ya moto.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuwalea watoto wa kike na kushughulika nao ni katika amali bora miogoni mwa amali njema zinazomuepusha mtu na moto.
  2. Sunna ya kutoa chochote kilicho ndani ya uwezo wa mtu hata kama ni kidogo.
  3. Huruma kubwa ya wazazi kwa watoto wao.
  4. Kumebainishwa hali ya nyumba za Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba riziki yake ilikuwa ya kumtosheleza pekee.
  5. Kumebainishwa fadhila za kujinyima kwa ajili ya watu wengine, na kwamba hilo ni katika alama za waumini; kwani Aisha alimpendelea yule mwanamke na watoto wake kuliko nafsi yake, na hii inaonyesha juu ya ukarimu wake na moyo wake wa kujitolea pamoja na kuwa ana uvihitaji.
  6. Zawadi ya watoto wa kike imeitwa kuwa ni mtihani; kwa sababu kuwalea kwake kuna shida na tabu nyingi, au kwa sababu ya baadhi ya watu kuwachukia, au ni kwa sababu mara nyingi wao huwa hawana vyanzo vya mapato ya maisha.
  7. Uislamu ulikuja kung'oa mizizi ya desturi mbovu za zama za ujinga, na miongoni mwake nikuwa uliusia watu kuwalea vizuri watoto wa kike.
  8. Mtu anapata malipo haya hata akiwa na binti mmoja kama ilivyokuja katika baadhi ya riwaya.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama