عن شداد بن أوس رضي الله عنه قال: ثِنْتَانِ حَفِظْتُهُمَا عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ اللهَ كَتَبَ الْإِحْسَانَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ، فَإِذَا قَتَلْتُمْ فَأَحْسِنُوا الْقِتْلَةَ، وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذَّبْحَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، فَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1955]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Shaddad bin Ausi -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Mambo mawili niliyahifadhi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisema:
"Hakika Mwenyezi Mungu amewajibisha (kufanya) wema katika kila kitu, mtakapoua basi ueni kwa namna iliyokuwa nzuri, na mtakapochinja basi kwa namna iliyokuwa nzuri, na anoe mmoja wenu zana yake ya kuchinjia, na akistareheshe kichinjwa chake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1955]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuwajibishia kutenda wema katika kila kitu, na wema: Ni kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu daima, na katika ibada zake, na katika kutenda kheri na kuacha kuwaudhi viumbe, miongoni mwa hayo ni kutenda wema katika kuuwa na kuchinja.
Wema katika kuuwa ni wakati wa kisasi: Achague njia nyepesi na rahisi zaidi na ya haraka zaidi kutoa roho kwa mwenye kuuawa.
Na wema katika kuchinja ni wakati wa kuchinja: Amuhurumie mnyama kwa kunoa kifaa, na kisinolewe mbele ya mnyama akitazama, na asichinjwe hali yakuwa wanyama wenzake wanatazama.