عن جابر رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«رَحِمَ اللهُ رَجُلًا سَمْحًا إِذَا بَاعَ، وَإِذَا اشْتَرَى، وَإِذَا اقْتَضَى».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 2076]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Jabiri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Allah amhurumie mtu ambaye ni mpole anapouza, na anaponunua, na anapo dai deni".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 2076]
Alimuombea rehema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila mwenye kuwa mwepesi mkarimu mpole katika biashara yake; Hamkadamizi mnunuzi katika bei yake, na anaamiliana naye kwa tabia njema, Mwepesi mkarimu mpole anaponunua; Hapunji na kupunguza thamani ya bidhaa, Mwepesi mkarimu mpole anapodai kulipwa madeni yake; hamtilii mkazo fukara na muhitaji, bali anamdai kwa upole na huruma, na anampa muda mwenye hali ngumu.