عن أبي كريمة المقداد بن معد يكرب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إِذَا أَحَبَّ الرَّجُلُ أَخَاهُ، فَلْيُخْبِرْهُ أَنَّهُ يُحِبُّهُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في السنن الكبرى وأحمد]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Karima Mikidadi bin Ma'di Yakrib-radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie- Amesema: "Atakapo mpenda mtu ndugu yake basi amwambie kuwa anampenda".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy

Ufafanuzi

Hadithi nyingi zimehimiza katika kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu-, na zikaeleza malipo yake, na hadithi hii inaashiria juu ya maana muhimu inayoweza kuleta athari kubwa katika mahusiano ya waumini baadhi yao kwa baadhi, kama jinsi inavyosambaza mapenzi, nayo ni mtu kumwambia ndugu yake kuwa anampenda, na hii inaonyesha kuhifadhi juu ya kuijenga jamii kutokana na sababu za kuisambaratisha na kuidhoofisha; na hii ni katika upande wa kusambaza mapenzi kati ya mtu mmoja mmoja katika jamii ya kiislamu, na kuyapa nguvu mahusiano ya jamii kwa udugu wa kiislamu, na haya yote yanatimia kwa kufanya sababu za mapenzi kama kubadilishana habari za kupendana kati ya wale wenye kupendana kwaajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Atakaye mpenda ndugu yake kwa ajiliya Mwenyezi Mungu basi na amueleze.
  2. Faida ya kumueleza nikuwa yeye atakapojua kuwa anampenda atakubali hata nasaha zake katika yale atakayomuelekeza katika uongofu wake, na hatoikataa kauli yake katika yale aliyomlingania katika wema uliofichika kwake.
  3. Ni sunna kumueleza aliyependwa kwaajili ya Mwenyezi Mungu kumpenda kwake, ili mapenzi yaongezeke na kuzoeana pia.