عن أبي هريرة رضي الله عنه : أن رجلًا قال للنبي -صلى الله عليه وآله وسلم-: أوصني، قال لا تَغْضَبْ فردَّدَ مِرارًا، قال لا تَغْضَبْ».
[صحيح] - [رواه البخاري]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za allah zimwendee- akisimulia kutoka kwa mtume: Kwamba mtu mmoja alimwambia Mtume -Rehma na amani ziwe juu yake- Niusie, Akasema: Usighadhibike, akarudiarudia swali na Mtume naye akaendelea kumwambia: Usighadhibike"
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy

Ufafanuzi

Mmoja wa maswahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- alimtaka Mtume -Rehma na amani ziwe juu yake- amuamrishe jambo ambalo litamfaa katika dunia na akhera, Mtume akamuambia asiwe mwenye hasira, na katika wasia wake huo aliposema " Usikasirike" unaondosha shari nyingi za watu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Pupa ya maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao juu yale yenye kuwanufaisha, kwa kauli yake: "Niusie".
  2. Kumtibu kila mwenye ugonjwa kwa kile kinachoendana na ugonjwa wake, kama itakuwa ni sahihi kuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake alimuelekezea huyu bwana nasaha hizi kwasababu yeye alikuwa ni mwingi wa hasira.
  3. Kutahadhari na hasira kwasababu ndizo zinazokusanya shari zote, na kujilinda nazo ndiyo kukusanya kheri zote.
  4. Kuamrishwa tabia ambazo akijipamba nazo mtu na zikawa kwake kama mazoea zitamzuilia hasira pale zinapotokea sababu za kukasirika, kama ukarimu na kujitolea, na upole na aibu, na mengineyo.
  5. Katika Mazuri ya dini ya kiislamu, nikuwa yenyewe inakataza tabia mbaya.
  6. Kufaa kutaka usia kutoka kwa mwenye elimu.
  7. Kufaa kutaka ziada katika usia.
  8. Hapa kuna ushahidi kwa kanuni ya 'kuziba njia' za kuleta madhara.
  9. kuna ushahidi wa yale aliyopendelewa Mtume katika ufasaha wa mazungumzo.
  10. Kukataza jambo ni kukataza pia sababu zake, na nikuamrisha pia njia zinazoweza kusaidia kuliacha.