عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«لَا ضَرَرَ وَلَا ضِرَارَ، مَنْ ضَارَّ ضَرَّهُ اللَّهُ، وَمَنْ شَاقَّ شَقَّ اللَّهُ عَلَيْهِ».
[صحيح بشواهده] - [رواه الدارقطني] - [سنن الدارقطني: 3079]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye".
[Ni sahihi kwa ushahidi wake] - [Imepokelewa na Addaar- Alqutni] - [سنن الدارقطني - 3079]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine,ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa.
Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka.
Kisha akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- adhabu pale yanapotokea madhara kwa mtu mwenye kuwadhuru watu, na pale zinapotokea tabu kwa mtu mwenye kuwatia watu tabu.