+ -

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا وَجَدَ أَحَدُكُمْ فِي بَطْنِهِ شَيْئًا، فَأَشْكَلَ عَلَيْهِ أَخَرَجَ مِنْهُ شَيْءٌ أَمْ لَا، فَلَا يَخْرُجَنَّ مِنَ الْمَسْجِدِ حَتَّى يَسْمَعَ صَوْتًا، أَوْ يَجِدَ رِيحًا».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 362]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapo hisi mmoja wenu chochote tumboni kwake, akapata wasi wasi, je kuna chochote kimemtoka au la?, basi asitoke msikitini mpaka asikie sauti, au anuse harufu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 362]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kitakapotatiza chochote tumboni kwa mwenye kusali, akapata shaka, je kuna chochote kimemtoka au la?, asiondoke katika swala yake na akaikatisha kwa ajili ya kurudia udhu, mpaka apate uhakika wa kutenguka udhu wake; ima kwa kusikia sauti ya upepo, au anuse harufu; kwa sababu mwenye uhakika habatilishi uhakika wake kwa shaka, hali yakuwa ana uhakika na twahara, na hadathi (kutengukwa udhu) kunatiliwa shaka.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, na ni kanuni miongoni mwa kanuni za kisheria, nayo ni; Yakini haiondoki kwa shaka, na asili ni kubaki hali iliyokuwa kama ilivyokuwa, mpaka mtu apate uhakika wa kinyume chake.
  2. Shaka haiathiri katika twahara, na mswaliji ataendelea kubaki katika twahara yake madama hajapata uhakika wa hadathi (kutengukwa udhu).