Orodha ya Hadithi

Mambo ya kimaumbile ni matano: Kutairiwa, na kuondoa nywele za sehemu ya siri, na kupunguza masharubu, na kupunguza kucha, na kukwapua nywele za kwapani.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Haikubali Mwenyezi Mungu swala ya mmoja wenu atakapotengukwa udhu mpaka atawadhe.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu, yatatoka madhambi yake mwilini mwake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Jisafisheni vizuri kutokana na mkojo; kwani adhabu nyingi za kaburini zinatokana na hilo.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Twahara (usafi) ni sehemu ya imani
عربي Lugha ya kiingereza Kiispania
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema; ziache; kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi, akafuta juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Yakwamba Fatuma bint Abii Hubaishi: Alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akasema: Hakika mimi napata hedhi na wala sitwahariki, je niache swala? Akasema: Hapana usiache sala, Hakika huo niupasukaji wa mshipa, lakini acha swala kiasi cha siku ambazo ulikuwa ukiingia katika hedhi, kisha oga na uswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke puani mwake maji, kisha apenge, na atakayestanji kwa mawe basi ayafanye kuwa witiri, na atakapoamka mmoja wenu toka usingizini mwake basi na aoshe mikono yake kabla hajaiingiza katika chombo mara tatu, kwani hakika mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapoamka asubuhi anasukutua kinywa chake kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaenda haja ndogo, akatawadha, na akafuta juu ya khufu zake (viatu vya ngozi mfano wa soksi).
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtakapokwenda haja kubwa, msielekee kibla kwa haja kubwa wala ndogo, na wala msikipe kibla mgongo, lakini elekeeni mashariki au magharibi.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Asishike mmoja wenu utupu wake kwa mkono wake wa kulia akiwa anakidhi haja ndogo, na asijifute haja ndogo au kubwa kwa mkono wake wa kulia na asipumulie ndani ya chombo anachonywea.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Atakapokunywa mbwa katika chombo cha mmoja wenu basi akioshe mara saba
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najilinda kwako kutokana na mashetani wa kiume na mashetani wa kike.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Kiliwekwa kwaajili ya Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- chombo cha kuogea janaba, akamimina kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto mara mbili -au tatu- kisha akaosha tupu yake, kisha akapiga ardhi kwa mkono wake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Alikuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- anapooga janaba, anaosha mikono yake kisha anatawadha udhu wake wa swala kisha anaoga
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilikuwa ni mtu mwenye madhii mengi, nikaona haya kumuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwasababu ya nafasi ya binti yake kwangu, nikamtuma Mikidadi bin Aswadi akamuuliza, akasema: Ataosha tupu yake, na atatawadha
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimshuhudia Amru bin Abii Hasan alimuuliza Abdullah bin Zaidi kuhusu udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- akaagiza bakuli la maji, akatawadha kwaajili yao udhu wa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Nilimjia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- naye akiwa anapiga mswaki kwa mswaki wa mti mbichi, Akasema: na ncha ya mswaki ikiwa katika ulimi wake, naye akisema: AAGH, AAGH (sauti ya kujigogoa), na mswaki ukiwa mdomoni mwake, kana kwamba anajigogoa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Hakika inakutosheleza kusema kwa mikono yako hivi: kisha akapiga kwa mikono yake miwili chini ya ardhi mpigo mmoja, kisha akapaka mkono wa kulia kwa kutumia mkono wa wa kushoto, na akapaka juu ya viganja vyake na uso wake.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Adhabu kali ya moto itazipata nyayo za miguu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Ni kwa jambo lipi alikuwa akianza nalo Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Anapoingia nyumbani kwake? Akasema: kwa mswaki
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Mambo kumi ni katika maumbile: Kupunguza masharubu, na kuziachia ndevu,na kupiga mswaki, na kupandisha maji puani, na kupunguza kucha, na kuosha fundo za vidole, na kunyofoa nywele za makwapani, na kunyoa nywele za sehemu za siri, na kustanji kwa maji.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anapiga katika kila fundo: Unatakiwa kulala usiku mrefu basi lala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa
Tulikuwa tukimuandalia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- mswaki wake na (maji yake kwaajili ya) twahara, basi Mwenyezi Mungu anamuamsha kwa muda anaotaka aamke nyakati za usiku, anapiga mswaki, na anatawadha na anaswali
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa