+ -

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ:
كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَانْتَهَى إِلَى سُبَاطَةِ قَوْمٍ، فَبَالَ قَائِمًا، فَتَنَحَّيْتُ فَقَالَ: «ادْنُهْ» فَدَنَوْتُ حَتَّى قُمْتُ عِنْدَ عَقِبَيْهِ فَتَوَضَّأَ فَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 273]
المزيــد ...

Kutoka kwa Hudhaifa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Nilikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akafika katika jalala la watu fulani akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, nikasimama kando naye, alipomaliza akasema: “Sogea karibu” nikasogea mpaka nikasimama karibu naye, akatawadha, kisha akapangusa juu ya soksi (Khufu) zake.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 273]

Ufafanuzi

Imepokelewa kutoka kwa Hudhaifa bin Al-Yaman kwamba alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akataka kukidhi haja ndogo, akaingia dampo la watu fulani; Napo ni mahali ambapo takataka na uchafu unaofagiliwa kutoka majumbani hutupwa hapo, hivyo akakidhi haja ndogo akiwa kasimama, na huwa anakidhi haja ndogo akiwa kachuchumaa.
Basi Hudhaifa akajisogeza mbali naye, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamwambia: Njoo karibu, basi Hudhaifa akamkaribia mpaka akasimama nyuma yake, nyuma ya miguu yake; Ili awe kama mstara kwake kutokana na watu kumtazama katika hali ile.
Kisha akatawadha, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, na wakati wa kuosha miguu yake, alitosheka kwa kupangusa juu ya soksi (Khofu) zake - nazo ni zile zinazovaliwa miguuni, zilizotengenezwa kwa ngozi nyembamba na mfano wake na zinazofunika vifundo vya miguu, na wala hakuzivua.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kupangusa juu ya Khufu (Soksi) mbili.
  2. Inafaa kukidhi haja wima, kwa sharti asidondokewe na chochote.
  3. Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alichagua Jalala, ambapo ni mahali pa kutupia taka za wafagiaji, kwa sababu huwa ni rahisi, na haja ndogo huwa hairudi tena kwa mkojoaji.