عَنْ إِبرَاهِيمَ النَّخَعِيِّ عَنْ هَمَّامِ بنِ الحَارِثِ قَالَ:
بَالَ جَرِيرٌ، ثُمَّ تَوَضَّأَ، وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ، فَقِيلَ: تَفْعَلُ هَذَا؟ فَقَالَ: نَعَمْ، رَأَيْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَالَ، ثُمَّ تَوَضَّأَ وَمَسَحَ عَلَى خُفَّيْهِ. قَالَ الأَعْمَشُ: قَالَ إِبْرَاهِيمُ: كَانَ يُعْجِبُهُمْ هَذَا الحَدِيثُ؛ لِأَنَّ إِسْلَامَ جَرِيرٍ، كَانَ بَعْدَ نُزُولِ المَائِدَةِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 272]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ibrahim Nakhai kutoka kwa Hammamu bin Harithi amesema:
Alikwenda haja ndogo Jariri kisha akatia udhu, na kafuta juu ya khufu zake, wakasema: Kwa nini unafanya hivi? Akasema: Ndio, Nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatia udhu na kafuta juu ya khufu zake. Amesema A'mashi: Amesema Ibrahimu: Ilikuwa ikiwashangaza sana hadithi hii; kwa sababu kusilimu kwa Jariri kulikuwa baada ya kuteremka Suratul-Maaida.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 272]
Alikidhi haja ndogo Jariri bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake kisha akatawadha, na akatosheka na kufuta juu ya khofu zake na hakuosha miguu yake, wakasema kumwambia walioko nao: Mbona unafanya hivi?! Akasema: Ndio, nilimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alikidhi haja ndogo, kisha akatawadha na akafuta juu ya khofu zake. Na Jariri alisilimu kwa kuchelewa baada ya kuteremka kwa suratul-Maaida ambayo ndani yake ina aya ya udhu, akiashiria kuwa kufuta juu ya khufu hakukufutwa kwa aya hiyo.