+ -

عَنْ جَابِرِ بْنِ سَمُرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا صَلَّى الفَجْرَ جَلَسَ فِي مُصَلَّاهُ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ حَسَنًا، وَقَالَ: كَانَ لَا يَقُومُ مِنْ مُصَلَّاهُ الَّذِي يُصَلِّي فِيهِ الصُّبْحَ أَوِ الغَدَاةَ، حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، فَإِذَا طَلَعَتِ الشَّمْسُ قَامَ، وَكَانُوا يَتَحَدَّثُونَ فَيَأْخُذُونَ فِي أَمْرِ الجَاهِلِيَّةِ، فَيَضْحَكُونَ وَيَتَبَسَّمُ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 670]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jabiri bin Samura radhi za Allah ziwe juu yake:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza vizuri, na akasema: Alikuwa hanyanyuki kutoka katika mswala wake alioswalia hapo Alfajiri au asubuhi, mpaka linapochomoza Jua, basi linapochomoza Jua anasimama, na walikuwa wakizungumza wanajikuta wameingia katika mazungumzo ya zama za ujinga, wanacheka na yeye anatabasamu.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 670]

Ufafanuzi

Na miongoni mwa sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwa anaposwali Alfajiri anakaa katika mswala wake mpaka Jua linachomoza kwa kunyanyuka, na alikuwa hasimami kutoka katika mswala wake aliouswalia Alfajiri, mpaka Jua lichomoze. Jua linapochomoza anasimama, na walikuwa wakizungumza wanachukua katika baadhi ya mambo yao ya kabla ya Uislamu na huku yeye kanyamaza, wanacheka, na huenda yeye akatabasamu pamoja nao.

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya kufanya dhikiri asubuhi mpaka Jua lichomoze, na kubaki katika kikao chake anapokuwa hana udhuru.
  2. Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa tabia njema na upole, kiasi kwamba alikuwa akikaa na Maswahaba zake, na akisikiliza mazungumzo yao na simulizi zao, na anatabasamu kwa sababu yake.
  3. Inafaa kufanya mazungumzo na kukumbushia enzi za ujinga msikitini.
  4. Inafaa kucheka na kutabasamu; kwa sababu kilichokatazwa ni kukithirisha kucheka.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama