عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا تَمْنَعُوا إِمَاءَ اللَّهِ مَسَاجِدَ اللَّهِ، وَلَكِنْ لِيَخْرُجْنَ وَهُنَّ تَفِلَاتٌ».
[حسن] - [رواه أبو داود] - [سنن أبي داود: 565]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Abuu Daud] - [سنن أبي داود - 565]
Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake msimamizi wa mwanamke na muhusika wake kuwakataza wanawake kwenda Msikitini, na akawaamrisha wanawake wakati wa kutoka kwenda Msikitini watoke bila kujipuliza manukato na wasitoke kwa kujiachia kwa mapambo; ili wasiwe sababu ya fitina kwa wanaume.