عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمْ المَسْجِدَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ اعْصِمْنِي مِنْ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ»، وَلِلْحَاكِمِ: «وَإِذَا خَرَجَ فَلْيُسَلِّمْ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ أَجِرْنِي مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ».
[حسن] - [رواه ابن ماجه والحاكم] - [سنن ابن ماجه: 773]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakapoingia mmoja wenu Msikitini basi amtakie rehema Mtume kisha aseme: Allaahummaf-tahlii abwaaba rahmatika, (Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: Allaahumma'swimnii minash-shaitwaanir-rajiim", (Ewe Mwenyezi Mungu nikinge dhidi ya Shetani aliyelaaniwa. Na katika riwaya ya Al-Haakim: "Na akitoka amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na aseme: Ewe Mwenyezi Mungu nilinde dhidi ya Shetani aliyelaaniwa".
[Ni nzuri] - [رواه ابن ماجه والحاكم] - [سنن ابن ماجه - 773]
Amemuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Muislamu atakapotaka kuingia Msikitini amtakie rehema Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa kusema: Allaahumma swalli alaa Muhammadi, kisha aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nifungulie milango ya rehema zako". Na akitoka amtakie rehema Mtume na aseme: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na shetani aliyelaaniwa", na katika riwaya nyingine ya imamu Hakim: Na aseme: "Awe Mwenyezi Mungu nilinde na Shetani aliyelaaniwa".