+ -

عَنْ ‌مَحْمُودِ بْنِ لَبِيدٍ رضي الله عنه:
أَنَّ ‌عُثْمَانَ بْنَ عَفَّانَ أَرَادَ بِنَاءَ الْمَسْجِدِ فَكَرِهَ النَّاسُ ذَلِكَ، وَأَحَبُّوا أَنْ يَدَعَهُ عَلَى هَيْئَتِهِ، فَقَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ بَنَى مَسْجِدًا لِلهِ بَنَى اللهُ لَهُ فِي الْجَنَّةِ مِثْلَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 533]
المزيــد ...

Kutoka kwa Mahmud bin Labidi radhi za Allah ziwe juu yake:
Anasimulia kuwa Othman bin Affan alitaka kujenga msikiti watu hawakulipenda swala hilo, na wakapendelea auache katika muonekano wake, akasema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Atakayejenga msikiti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu atamjengea Peponi nyumba mfano wake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 533]

Ufafanuzi

Othman bin Affan alitaka kuujenga msikiti wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa sura nzuri zaidi kuliko jengo lake la awali, watu hawakupendezwa na swala hilo; kwa sababu msikiti utabadilika kutoka katika muonekano wa jengo lake lilivyokuwa katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, msikiti ulikuwa umejengwa kwa matofali, na paa lake lilikuwa limeezekwa kwa makuti, lakini Othman alitaka kuujenga kwa mawe na chokaa, Othman radhi za Allah ziwe juu yake akawaeleza kuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: Atakayejenga msikiti kwa kutafuta radhi zake Mtukufu, si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, Mwenyezi Mungu atamlipa malipo bora kulingana na amali yake, na malipo hayo ni Mwenezi Mungu kumjengea mfano wake peponi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kujenga misikiti na fadhila zake.
  2. Kupanua msikiti na kuukarabati yote haya yanaingia katika fadhila za kujenga.
  3. Umuhimu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.