عَنْ أَبِي حُمَيْدٍ أَوْ عَنْ أَبِي أُسَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 713]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 713]
Ameuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.