+ -

عن عائشة رضي الله عنها عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«إِنَّ أَبْغَضَ الرِّجَالِ إِلَى اللهِ الْأَلَدُّ الْخَصِمُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 2457]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakika mtu anayechukiza zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni mgomvi mkorofi".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 2457]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- anawachukia miongoni mwa watu mwenye ugomvi mkali na mwingi, asiyekubali kutii haki, na anajaribu kuikataa kwa mijadala, au akagombana kwa haki akapitiliza katika ugomvi na akatoka katika mpaka wa uadilifu, na akajadiliana bila elimu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Haingii katika mlango wa mgomvi mbaya, aliyedhulumiwa kudai haki yake kwa njia ya kushitakiana kisheria.
  2. Mijadala na ugomvi ni katika maafa ya ulimi yanayosababisha kutengana na kupeana migongo kati ya waislamu.
  3. Mjadala ni mzuri utapokuwa katika haki na utaratibu mzuri, na unakuwa mbaya utapokuwa ni kwa kuikataa haki na kuitetea batili, au ukawa bila hoja wala ushahidi.