عن أبي أيوب الأنصاري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «لا يحل لمسلم أن يهجر أخاه فوق ثلاث ليال، يلتقيان: فيُعرض هذا، ويُعرض هذا، وخيرهما الذي يبدأ بالسلام».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abii Ayubu An Answariy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Si halali kwa muislamu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana: huyu anampuuza huyu, na huyu anampuuza huyu, na mbora wao ni yule anayeanza kwa salamu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Katika hadithi kuna katazo la kumhama muislamu ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote wawili kila mmoja akampuuza mwenzie na wala hamsalimii wala hamsemeshi, na inafahamika pia kutoka katika kauli hii uhalali wa kumhama mtu chini ya siku tatu, kwa kuzingatia tabia za kibinadamu, kwasababu mwanadamu ameumbwa na hasira, na tabia mbaya, akasamehewa kumhama mwenzie ndani siku tatu, ili litoweke lile lililojitokeza baina yao, na makusudio ya kuhama katika hadithi ni kuhama kwasababu ya maslahi ya nafsi, ama kuhama kwasababu ya haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu, na watu wa uzushi, na marafiki waovu, swala hili halina muda maalumu, bali linaambatana na sababu ambayo litaondoka kwa kuondoka kwake, na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kutengana huku, kwa kuanza kwa salamu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa kumhama muislamu zaidi ya siku tatu, katika yale yanayohusiana na mambo ya kidunia.
  2. Ubora wa yule anayemuanza mwenzie kwa salamu, na akaondoa kile kilicho kati yao miongoni mwa kuhamana na kutengana.
  3. Ubora wa salamu, nakuwa inaondoa yaliyomo ndani ya nafsi, na kuwa ni alama ya upendo.