عن جُبَير بن مُطْعِم رضي الله عنه أنه سمع النبي صلى الله عليه وسلم يقول:
«لَا يَدْخُلُ الْجَنَّةَ قَاطِعُ رَحِمٍ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2556]
المزيــد ...

Kutoka kwa Jubairi bin Mutwim -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Haingii peponi mkata udugu".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake] - [Swahiih Muslim - 2556]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa atakayewakatia ndugu zake wa karibu zile haki za wajibu kwao, au akawaudhi au kuwafanyia ubaya, basi anastahiki asiingie peponi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kukata udugu ni dhambi kubwa katika madhambi makubwa.
  2. Kuunga udugu kunakuwa kulingana na desturi za watu, na kutatofautiana kulingana na mazingira na zama na jamii pia.
  3. Kuunga udugu kunakuwa kwa kutembeleana, na kwa sadaka, na kuwatendea wema, na kuwatembelea wagonjwa, na kuwaamrisha mema, na kuwakataza maovu, na mengineyo.
  4. Kila ambavyo kukata udugu kunavyozidi kuwa kwa ndugu wa karibu zaidi ndivyo ambavyo madhambi yanavyokuwa makubwa.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (66)