عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه:
أَنَّ رَجُلًا قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ إِنَّ لِي قَرَابَةً أَصِلُهُمْ وَيَقْطَعُونِي، وَأُحْسِنُ إِلَيْهِمْ وَيُسِيئُونَ إِلَيَّ، وَأَحْلُمُ عَنْهُمْ وَيَجْهَلُونَ عَلَيَّ، فَقَالَ: «لَئِنْ كُنْتَ كَمَا قُلْتَ، فَكَأَنَّمَا تُسِفُّهُمُ الْمَلَّ وَلَا يَزَالُ مَعَكَ مِنَ اللهِ ظَهِيرٌ عَلَيْهِمْ مَا دُمْتَ عَلَى ذَلِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2558]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakwamba mtu mmoja alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mimi nina ndugu wa karibu, ninawaunga lakini wao wananitenga, ninawafanyia wema lakini wao wanatendea ubaya, na ninakuwa mpole kwao lakini wao wananifanyia ujeuri, basi akasema: "Ikiwa kama utakuwa kama ulivyosema, basi ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto (dhambi wanazozipata ni kama mtu anayekula majivu ya moto), na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, madam bado uko katika hali hiyo".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2558]
Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ana ndugu wa karibu wa ukoo anaamiliana nao kwa wema ila wao wanaamiliana naye kinyume na hivyo; anawaunga na kuwatembelea ila wao wanamtenga, na anawatendea ihisani kwa wema na uadilifu ila wao wanamtendea ubaya kwa ujeuri na ukaidi, na anakuwa mpole kwao na kuwasamehe ila wao wanampuuza kwa kumfanyia mabaya katika kauli na vitendo, je, aendelee kuwaunga udugu pamoja na hayo yote yaliyotajwa?
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ikiwa ni hivyo kama ulivyoeleza basi wewe unawafedhehesha na kuwadharaulisha katika nafsi zao, ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto; kwa wingi wa wema wako na kwa ubaya wa matendo yao mbele ya nafsi zao, na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, na wao waendelee katika kukutendea ubaya.