عن أبي الدرداء رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ رَدَّ عَنْ عِرْضِ أَخِيهِ رَدَّ اللهُ عَنْ وَجْهِهِ النَّارَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ».

[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 1931]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Dardaa -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayeitetea heshima ya ndugu yake basi Mwenyezi Mungu ataukinga uso wake na moto siku ya Kiyama".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad] - [Sunanu Tirmidhiy - 1931]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeitetea heshima ya ndugu yake muislamu akiwa hayupo (katika mazungumzo) kwa kukataza watu kumsema vibaya na kumkosea adabu, basi naye Mwenyezi Mungu ataizuia adhabu kwake siku ya Kiyama.

Katika Faida za Hadithi

  1. Katazo la kuzungumza kuhusu heshima za waislamu.
  2. Malipo huendana na matendo, atakayeirudisha heshima ya ndugu yake Mwenyezi Mungu naye atauzuia moto kwake.
  3. Uislamu ni dini ya udugu na kuteteana kati ya waislamu.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)