عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «ما نقصت صدقة من مال، وما زاد الله عبدا بعفو إلا عزا، وما تواضع أحد لله إلا رفعه الله عز وجل »
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yakwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Haijawahi kupunguza sadaka chochote katika mali, Na hajawahi kumzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa usamehevu (wake) ispokuwa utukufu, na hajawahi kunyenyekea yeyote ispokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimnyanyua".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
(Haijawahi kupunguza sadaka chochote katika mali) Maana yake nikuwa: sadaka inapotolewa basi haipunguzi mali bali inaizidisha, na inaitia baraka, na inaizuilia maafa, kuzidi kwa mali ima kiwango: kwa kumfungulia Mwenyezi Mungu mja milango ya riziki, au namna: kwa kuiteremshia Mwenyezi Mungu baraka ambayo inaizidisha kwa kadiri ya kile alichokitoa katika sadaka. Na hamuongezei Mwenyezi Mungu mja kwa usamehevu wake ispokuwa utukufu, yaani: nikuwa mwenye kujua faida za kusamehe na akaacha kuadhibu na kulaumu, basi atapata heshima na utukufu katika nyoyo, na ataongeza utukufu na karama, na kupandishwa daraja duniani na akhera. Na hajawahi kunyenyekea mja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ispokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua, Maana yake nikuwa mwenye kujidhalilisha kwa Mwenyezi Mungu na akaonyesha unyonge mbele yake Aliyetakasika na kutukuka, na akawa mlaini katika upande wa viumbe, na akaonyesha unyonge kwa waislamu, basi sifa hizi hazimuongezei mwenye kujipamba nazo ispokuwa ni kunyanyuliwa daraja duniani na akhera na mapenzi katika nyoyo, na nafasi ya juu peponi.