عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قالَ: قالَ رَسُولُ اللَّهِ صلَّى اللَّهُ عليْه وسلَّمَ:
«دِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ فِي رَقَبَةٍ، وَدِينَارٌ تَصَدَّقْتَ بِهِ عَلَى مِسْكِينٍ، وَدِينَارٌ أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ أَعْظَمُهَا أَجْرًا الَّذِي أَنْفَقْتَهُ عَلَى أَهْلِكَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 995]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 995]
Ametaja Mtume rehema na amani ziwe juu yake baadhi ya aina za utoaji, akasema: Dinari uliyoitoa katika Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari uliyoitoa katika shingo ya mtumwa, na dinari uliyoitoa sadaka kwa masikini mwenye uhitaji, na dinari uliyoitoa kwa watu wako na familia yako, kisha akaeleza kuwa yenye malipo makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ile uliyoitoa kwa watu wako na familia na wale wanaokulazimu kuwahudumia.