عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«قَالَ اللهُ: أَنْفِقْ يَا ابْنَ آدَمَ أُنْفِقْ عَلَيْكَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5352]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Toa ewe mwanadamu na mimi nikupe".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake] - [Swahiih Al Bukhaariy - 5352]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Toa ewe mwanadamu -katika matumizi ya wajibu na ya hiyari- nikukunjulie na nikupe badala ya hicho na nikubariki ndani yake.