عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ رَجُلًا سَأَلَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ الإِسْلاَمِ خَيْرٌ؟ قَالَ: «تُطْعِمُ الطَّعَامَ، وَتَقْرَأُ السَّلاَمَ عَلَى مَنْ عَرَفْتَ وَمَنْ لَمْ تَعْرِفْ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 12]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah Bin Amri -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-:
Ya kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume rehema na amani zimfikie: Ni Uislamu upi bora? Akasema: "Ni, ulishe chakula, na utoe salamu kwa unayemjua na usiyemjua".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 12]
Aliulizwa Mtume rehema na amani zimfikie: Ni jambo lipi katika Uislamu ni bora? Akataja mambo mawili:
La kwanza: Kukirithirisha kuwalisha masikini, na inaingia hapa sadaka na zawadi na kuwakirimu wageni na walima (harusi), na inatiliwa mkazo fadhila ya kulisha masikini katika nyakati za njaa na wakati wa bidhaa kupanda bei.
La pili: Kumpa salamu kila muislamu, unayemjua na usiyemjua.