عن أبي هريرة رضي الله عنه : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:«حقُّ المُسلمِ على المُسلمِ خمسٌّ: ردُّ السلام، وعِيَادَةُ المريض، واتباع الجنائز، وإجابة الدَّعوة، وتَشميتُ العاطِس».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake Amesema: "Haki za Muislamu juu ya muislamu ni tano: Kujibu salamu, na kumtembelea mgonjwa, na kusindikiza jeneza, na kuitika wito, na kumtakia rehma mwenye kupiga chafya".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Katika hadithi hii kumebainishwa baadhi ya haki za muislamu juu ya muislamu mwenzie, na haki za muislamu kwa ndugu yake ni nyingi, lakini Mtume rehema na Amani ziwe juu yake wakati mwingine anataja vitu maalumu miongoni mwa vingi; kwa kuvipa kipaumbele na kwa kutosheka na hivyo, na katika hayo ni yale aliyoyataja Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, yakwamba yeye Amesema: "Haki za muislamu juu ya muislamu ni tano: kujibu salamu: Yaani anapokusalimia mjibu, na katika hadithi nyingine: "Haki za muislamu juu ya muislamu ni sita: ukikutana naye msalimie".Haki hizi yeyote atakaye zisimamia katika haki za waislamu kwa namna inayotakiwa, itakuwa kwake kusimamia zisizokuwa hizi ndio bora zaidi, na atakuwa ametekeleza wajibu huu na haki ambazo ndani yake kuna kheri nyingi na malipo makubwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu atakapotaraji malipo ya hilo toka kwa Mwenyezi Mungu.Ya kwanza katika haki hizi: "Ukikutana naye msalimie" Na katika hadithi nyingine "Jibu salamu".Haki ya pili: Kumtembelea mgonjwa anapougua na akajitenga na watu nyumbani kwake au Hospitalini au kwingineko, basi ana haki kwa ndugu zake waislamu ya kumtembelea. Ama Haki ya tatu: Ni kufuata jeneza na kulisindikiza, kwani katika haki za muislamu juu ya ndugu yake alifuate jeneza lake toka nyumbani kwake mpaka mahali pa kuswaliwa sawa sawa iwe msikitini au sehemu nyingine mpaka makaburini. Haki ya nne: Ni kuitika wito, katika haki za muislamu juu ya ndugu yake anapomuita amuitikie. Haki ya tano: Kumtakia rehema anapopiga chafya: Hivyo ni kwasababu chafya ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu; kwa kutoka hewa ambayo ilikwama katika baadhi ya sehemu ya mwili wa mwanadamu, ameirahisishia Mwenyezi Mungu njia ikatoka akastarehe mwenye kupiga chafya, akawekewa sheria ya kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema hii, na akawekewa sheria ndugu yake amwambie: "Yar-hamukallaahu" akurehemu Mwenyezi Mungu, na akaamrishwa amjibu "Akuongozeni Mwenyezi Mungu na akunyoosheeni mambo yenu" Ambaye hatomshukuru Mwenyezi Mungu hatostahiki kuombewa rehma, na asimlaumu yeyote ila nafsi yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kubainishwa haki za Muislamu juu ya muislamu, miongoni mwazo: Kuna za wajibu, za sunna, na zinatofautiana kulingana na hali na watu.
  2. Kujibu salamu ni faradhi ya lazima atakapokuwa anayesalimiwa ni mmoja, na ni faradhi ya kujitosheleza watakapokuwa wengi.
  3. Kumtembelea mgonjwa ni faradhi ya kujitosheleza.
  4. Kulifuata jeneza ni faradhi ya kujitosheleza, nako ni Kulisindikiza kutoka mahala pake au mahala pa kuswaliwa mpaka sehemu ya maziko.
  5. Kuitika mwaliko wa harusi kwa sharti zake zilizowekwa katika vitabu vya sheria ni wajibu, na katika walima zote ni sunna iliyotiliwa mkazo.
  6. Kumtakia rehma aliyepiga chafya baada yakuwa amemshukuru Mwenyezi Mungu, Wamesema baadhi ya wanachuoni: Hilo ni wajibu uwajibu wa lazima kukiwa hakuna mtu mwingine, na ni wajibu wa kujitosheleza kwa watu wengi, na wamesema wengine: Ni sunna.
  7. Utukufu wa uislamu katika kutilia nguvu mahusiano ya kiudugu na mapenzi baina ya waislamu.
  8. Haifai kumtakia rehma aliyepiga chafya, wala kujibu salamu, imamu akiwa ana hutubu; kwasababu yote hayo mawili ni mazungumzo, na mazungumzo yameharamishwa katika hutuba.