عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«خَيْرُ يَوْمٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ، فِيهِ خُلِقَ آدَمُ، وَفِيهِ أُدْخِلَ الْجَنَّةَ، وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا، وَلَا تَقُومُ السَّاعَةُ إِلَّا فِي يَوْمِ الْجُمُعَةِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 854]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
“Siku bora zaidi iliyochomozewa jua ni siku ya Ijumaa, ndani yake aliumbwa Adam, na ndani yake aliingizwa Peponi, na ndani ya siku hii akatolewa humo, na hakitosimama Kiyama ila siku ya Ijumaa".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 854]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake anatueleza kuwa siku bora kabisa iliyochomozewa na jua ni Ijumaa, Miongoni mwa sifa zake: Mwenyezi Mungu alimuumba Adam, amani imshukie, na ndani yake akamuingiza Peponi, na ndani yake akamtoa na akamteremsha duniani, na Kiyama hakitosimama ila siku ya Ijumaa.