عن أبي موسى رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«إِنَّ اللهَ لَيُمْلِي لِلظَّالِمِ، حَتَّى إِذَا أَخَذَهُ لَمْ يُفْلِتْهُ» قَالَ: ثُمَّ قَرَأَ: «{وَكَذَلِكَ أَخْذُ رَبِّكَ إِذَا أَخَذَ الْقُرَى وَهِيَ ظَالِمَةٌ إِنَّ أَخْذَهُ أَلِيمٌ شَدِيدٌ}[هود: 102]»
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4686]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Musa -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Mwenyezi Mungu humpa muda dhalimu, mpaka akija kumuadhibu hambakishi" Anasema: Kisha akasoma: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika mkamato wake ni mchungu na mkali" [Hud:102]
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4686]
Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuendelea kubaki katika dhulma kwa kufanya maasi na ushirikina na kuwadhulumu watu haki zao, kwani Allah Mtukufu humpa muda dhalimu na humchelewesha na humpa umri mrefu na mali nyingi hamharakishii adhabu; ikiwa hatotubia basi humchukua mara moja na huwa hambakishi na huwa hamuachi kwa sababbu ya wingi wa dhulma zake.
Kisha akasoma -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Na hivyo ndivyo kuadhibu kwa Mola wako Mlezi anapoikamata miji inapokuwa imedhulumu. Hakika adhabu yake ni chungu na ni kali" [Hud:102]