عن أبي هريرة رضي الله عنه: أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«يَنْزِلُ رَبُّنَا تَبَارَكَ وَتَعَالَى كُلَّ لَيْلَةٍ إِلَى السَّمَاءِ الدُّنْيَا حِينَ يَبْقَى ثُلُثُ اللَّيْلِ الْآخِرُ، يَقُولُ: «مَنْ يَدْعُونِي فَأَسْتَجِيبَ لَهُ؟ مَنْ يَسْأَلُنِي فَأُعْطِيَهُ؟ مَنْ يَسْتَغْفِرُنِي فَأَغْفِرَ لَهُ؟».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1145]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Anateremka Mola wetu Mlezi -Aliyetakasika na kutukuka- katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, husema: "Ni nani anayeniomba nimjibu? Ni nani anayenitaka shida yake nimpe? Ni nani anayeniomba msamaha nimsamehe?".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1145]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka huteremka kila usiku katika mbingu ya dunia pindi inapobakia theluthi ya mwisho ya usiku, na anawahamasisha waja wake wamuombe, kwani yeye anamjibu mwenye kumuomba, na anawahimiza wamtake haja zao, kwani yeye humpa anayemuomba, na anawaita wamuombe msamaha kutokana na madhambi yao kwani yeye huwasamehe waja wake waumini.