عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ -وَكَانَ غَزَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثِنْتَيْ عَشْرَةَ غَزْوَةً- قَالَ: سَمِعْتُ أَرْبَعًا مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَعْجَبْنَنِي، قَالَ:
«لاَ تُسَافِرِ المَرْأَةُ مَسِيرَةَ يَوْمَيْنِ إِلَّا وَمَعَهَا زَوْجُهَا أَوْ ذُو مَحْرَمٍ، وَلاَ صَوْمَ فِي يَوْمَيْنِ: الفِطْرِ وَالأَضْحَى، وَلاَ صَلاَةَ بَعْدَ الصُّبْحِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، وَلاَ بَعْدَ العَصْرِ حَتَّى تَغْرُبَ، وَلاَ تُشَدُّ الرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلاَثَةِ مَسَاجِدَ: مَسْجِدِ الحَرَامِ، وَمَسْجِدِ الأَقْصَى، وَمَسْجِدِي هَذَا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1995]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa kapigana vita pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- takriban vita kumi na mbili (12) anasema: Nilisikia mambo manne kutoka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, yakanifurahisha sana, anasema:
"Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake (Ndugu asiyeweza kumuoa), hakuna kufunga ndani ya siku mbili: Idil Fitri na Idil Adh-ha, na hakuna swala baada swala ya Asubuhi mpaka lichomoze jua, na wala baada ya Lasiri mpaka lizame, na wala haifungwi safari isipokuwa katika misikiti mitatu: Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Aqswa (Palestina), na msikiti wangu huu (Madina)".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1995]
Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo manne:
La kwanza: Kamkataza mwanamke kusafiri mwendo wa siku mbili bila kuwa na mume wake au mmoja kati ya maharimu wake, naye ni mtu aliyeharamu kwake kumuoa uharamu wa moja kwa moja (usio wa moja kwa moja, kama mume wa dada yake) kama mwanaye, na baba, na mtoto wa kaka, na kijana wa dada, na baba mdogo au mkubwa, na mjomba, na mfano wake.
La pili: Katazo la kufunga siku Idil Fitri na siku ya Idil Adh-ha, sawa sawa muislamu amezifunga kwa udhuru au kwa kujitolea, au kafara.
La tatu: Amekataza kusali swala ya sunna baada ya swala ya Lasiri mpaka lizame Jua, na baada ya kuchomoza asubuhi mpaka lichomoze Jua.
La nne: Katazo la kusafiri kwenda eneo katika maeneo kwa itikadi kuwa kuna ubora, na kuitakidi kuwa kuna kulipwa malipo mengi, isipokuwa misikiti hii mitatu, hivyo hakuna kufunga safari kwenda misikiti isiyokuwa hiyo kwa ajili kuswali ndani yake, kwani malipo hayalipwi kwa wingi isipokuwa katika misikiti hii mitatu, Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Mtume (Madina), na Msikiti wa Aqswa (Palestina).