عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضيَ اللهُ عنهما:
أنَّهُ قَالَ لعَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ: أَلَا أُرِيكَ امْرَأَةً مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هَذِهِ الْمَرْأَةُ السَّوْدَاءُ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: إِنِّي أُصْرَعُ وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ، فَادْعُ اللهَ لِي، قَالَ: «إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ أَنْ يُعَافِيَكِ» قَالَتْ: أَصْبِرُ، قَالَتْ: فَإِنِّي أَتَكَشَّفُ فَادْعُ اللهَ أَنْ لَا أَتَكَشَّفَ، فَدَعَا لَهَا.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2576]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake:
Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2576]
Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.