عَنْ مَطَرِ بْنِ عُكَامِسٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا قَضَى اللَّهُ لِعَبْدٍ أَنْ يَمُوتَ بِأَرْضٍ جَعَلَ لَهُ إِلَيْهَا حَاجَةً».

[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2146]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Matwar Bin Ukaamis -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Mwenyezi Mungu akimpangia mja afie sehemu fulani humfanya ahitajie kitu sehemu ile."

[Sahihi] - [Imepokelewa Imamu Tirmidhiy] - [Sunanu Tirmidhiy - 2146]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: kuwa Mwenyezi Mungu akimpangia mtu kuwa afie katika ardhi fulani na hali yakuwa yeye hayupo katika ardhi hiyo; Basi humfanya ahitajie kitu katika ardhi ile hivyo ataenda katika ardhi ile, basi huchukuliwa roho yake akiwa huko.

Katika Faida za Hadithi

  1. Hadithi inathibitisha maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na nafsi haijui itafia katika ardhi gani."
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (65)