عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال: "إن عِظَمَ الجزاءِ مع عِظَمِ البلاءِ، وإن الله تعالى إذا أحب قوما ابتلاهم، فمن رَضِيَ فله الرِضا، ومن سَخِطَ فله السُّخْطُ".
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Anas bin Maliki radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, yakuwa yeye Amesema: "Hakika ukubwa wa malipo huendana sawa pamoja na ukubwa wa matatizo, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anapowapenda watu huwapa mtihani; atakayeridhia atapata radhi, na atakayechukia atapata hasira (za Mwenyezi Mungu)."
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah

Ufafanuzi

Anatueleza Mtume rehema na Amani ziwe juu yake- katika hadithi kuwa muumini linaweza kutokea kwake jambo lolote katika matatizo, katika nafsi yake au mali yake au kinginecho, nakuwa Mwenyezi Mungu atamlipa juu ya matatizo hayo ikiwa kama yeye atavumilia, nakuwa kila majanga yanavyozidi kuwa makubwa na hatari yake kuwa kubwa ndivyo malipo yake yanavyokuwa makubwa kwa Mwenyezi Mungu, kisha anabainisha rehema na Amani zimfikie kuwa mitihani ni katika alama za kuwapenda Mwenyezi Mungu waumini, nakuwa hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake ni lazima yafanyike hakuna namna, lakini atakayesubiri na akaridhia, basi Mwenyezi Mungu atamlipa kwa hilo kwa kumridhia na zinamtosha zaidi thawabu zake, nakuwa atakayechukia na akakerwa na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake, basi Mwenyezi Mungu atamchukia na zinamtosha zaidi adhabu zake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Nikuwa matatizo yanafuta madhambi, madam tu hajaambatana na kuacha la wajibu, kama kuacha kuvumilia, au kufanya la haramu kama kuchana nguo na kupiga mashavu.
  2. Kuthibitisha sifa ya mapenzi kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
  3. Hakika matatizo kwa Muumini ni katika alama za Imani.
  4. Kuthibitisha sifa ya kuridhia na kuchukia kwa Mwenyezi Mungu kwa namna inayoendana na Utukufu wake.
  5. Kupendeza kuridhika na hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
  6. kuharamishwa kukasirikia hukumu ya Mwenyezi Mungu na makadirio yake.
  7. Kuhimizwa kuvumilia juu ya matatizo.
  8. Mwanadamu anaweza kuchukia jambo nalo likawa na kheri.
  9. Kuthibitisha hekima kwa Mwenyezi Mungu katika vitendo vyake.
  10. Malipo huendana na matendo.