+ -

عَنْ طَاوُسٍ أَنَّهُ قَالَ: أَدْرَكْتُ نَاسًا مِنْ أَصْحَابِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، يَقُولُونَ كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، قَالَ: وَسَمِعْتُ عَبْدَ اللهِ بْنَ عُمَرَ رضي الله عنهما يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«كُلُّ شَيْءٍ بِقَدَرٍ، حَتَّى الْعَجْزِ وَالْكَيْسِ، أَوِ الْكَيْسِ وَالْعَجْزِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2655]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Twaausi kuwa yeye amesema: Niliwakuta watu miongoni mwa maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- wakisema kuwa kila kitu huwa kwa namna ilivyopangwa, akasema: Na nimemsikia Abdullah bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake- anasema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kila jambo linakuwa kwa namna lilivyopangwa, mpaka kushindwa kufanya jambo fulani au kulifanya kwa ufanisi, au kufanya kwa ufanisi au kushindwa kabisa kufanya."

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2655]

Ufafanuzi

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila jambo linakuwa kwa mujibu wa lilivyopangwa; Mpaka kushindwa: Nako nikuacha jambo ambalo ni wajibu kulifanya au kulichelewesha katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hata kufanya jambo kwa ufanisi: Nako ni kufanya kwa uchangamfu na weledi katika mambo ya kidunia au ya Akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu amepangilia jambo la kushindwa au kufanya kwa ufanisi na amepangilia kila kitu, hakuna chochote kinachotokea isipokuwa kinatokea kwa ujuzi wake Mwenyezi Mungu na kutaka kwake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Imewekwa wazi itikadi ya Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kuamini mipango ya Mwenyezi Mungu -Kadari-.
  2. Kila kitu kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu mpaka kushindwa na kuweza kufanya jambo.
  3. Uimara wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- katika kupokea na kufikisha maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake.
  4. Kuamini -Kadari- kheri zake na shari zake.