عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«كَتَبَ اللهُ مَقَادِيرَ الْخَلَائِقِ قَبْلَ أَنْ يَخْلُقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِخَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ، قَالَ: وَعَرْشُهُ عَلَى الْمَاءِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2653]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Amrou Bin Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Aliandika Mwenyezi Mungu makadirio ya viumbe kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, akasema: Na Arshi yake ilikuwa juu ya maji."
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2653]
Anatoa habari Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu aliandika mambo yote ambayo yatatokea miongoni mwa mambo ya kuwakadiria viumbe kwa uchanganuzi kuanzia kuishi na kufa na riziki na mambo mengineyo aliyaandika katika Lauhil Mah-fuudh kabla ya kuumba Mbingu na Ardhi kwa zaidi ya miaka elfu hamsini, na hayo aliyoyaandika hutokea kwa mujibu wa alivyopanga Hivyo basi kila kitu chenye kutokea, basi kinatokea kwa mipango ya Mwenyezi Mungu na kukadiria kwake. Basi jambo lolote linalompata mja lisingeweza kumkosa, na lenye kumkosa lisingeweza kumpata.