+ -

عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
حَدَّثَنَا رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَهُوَ الصَّادِقُ المَصْدُوقُ: «أَنَّ خَلْقَ أَحَدِكُمْ يُجْمَعُ فِي بَطْنِ أُمِّهِ أَرْبَعِينَ يَوْمًا وَأَرْبَعِينَ لَيْلَةً، ثُمَّ يَكُونُ عَلَقَةً مِثْلَهُ، ثُمَّ يَكُونُ مُضْغَةً مِثْلَهُ، ثُمَّ يُبْعَثُ إِلَيْهِ المَلَكُ، فَيُؤْذَنُ بِأَرْبَعِ كَلِمَاتٍ، فَيَكْتُبُ: رِزْقَهُ وَأَجَلَهُ وَعَمَلَهُ وَشَقِيٌّ أَمْ سَعِيدٌ، ثُمَّ يَنْفُخُ فِيهِ الرُّوحَ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ الجَنَّةِ حَتَّى لاَ يَكُونُ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ فَيَدْخُلُ النَّارَ، وَإِنَّ أَحَدَكُمْ لَيَعْمَلُ بِعَمَلِ أَهْلِ النَّارِ حَتَّى مَا يَكُونُ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ إِلَّا ذِرَاعٌ، فَيَسْبِقُ عَلَيْهِ الكِتَابُ، فَيَعْمَلُ عَمَلَ أَهْلِ الجَنَّةِ فَيَدْخُلُهَا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 7454]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
Ametuhadithia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- naye ni mkweli mwenye kukubaliwa: "Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake kwenye tumbo la mama yake mchana arobaini na nyusiku arobaini kisha anakuwa tone la manii kwa muda kama huo kisha anakuwa pande la damu kwa mfano wa siku hizo, kisha hutumwa Malaika na huamrishwa kufanya mambo manne; Hivyo basi ataandika riziki yake, na muda wa kufa kwake na matendo yake na ataandika kuwa ni muovu au ni mwema, kisha atampulizia roho, na kwa hakika mmoja wenu anaweza kufanya matendo ya watu wa Peponi kiasi ya kuwa haitobakia kati yake na kuingia Peponi isipokuwa usawa wa urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu -Kadari- na akafanya matendo ya watu wa motoni na akaingia motoni, na kwa hakika mmoja wenu anaweza akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa motoni mpaka ikabakia kati yake na kuingia motoni kiasi cha usawa wa mkono kisha kikamtangulia kitabu -Kadari- akafanya mataendo ya watu wa peponi na akaingia peponi."

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 7454]

Ufafanuzi

Amesema Bin Masoud: Ametuhadithia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake naye ni mkweli kwenye maneno yake, na mwenye kukubaliwa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amemkubali, Amesema: Kwa hakika mmoja wenu hukusanywa umbile lake, na jambo hilo ni kuwa mtu akimuingilia mke wake basi yale manii yake yaliyosambaa hukusanywa kwenye tumbo la mwanamke kwa muda wa siku arobaini yakiwa ni tone la manii, Kisha hubadilika na kuwa pande la damu nzito iliyoganda, haya hufanyika katika arobaini ya pili, Kisha hubadilika kuwa pande la nyama, nacho ni kipande cha nyama chenye ukubwa wa kuweza kutafunwa, na mabadiliko haya ni katika arobaini ya tatu, Kisha Mwenyezi Mungu hulitumia pande hilo la nyama Malaika, kisha hulipulizia ndani yake roho baada ya kuisha siku arobaini za tatu, Na huamrishwa Malaika aandike maneno manne, nayo ni: Riziki yake, nacho ni kiwango ambacho atakipata miongoni mwake ni neema katika umri wake, Na pia huandikwa wakati wake, nao ni muda wa kubakia kwake Duniani, Na matendo yake, yatakuwa ni yapi? Na je atakuwa muovu au mwema. Kisha akaapa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yawezekana mtu akafanya matendo miongoni mwa matendo ya watu wa peponi, na yakawa matendo yake ni mazuri, yaani kwenye muonekano wa watu, na akabakia hivyo mpaka inakuwa kati yake na Pepo ni kiasi cha mkono, yaani kiasi kilichobaki kati yake mpaka kuifikia pepo ni kidogo sana kama vile ambavyo mtu amebakiza nafasi kati yake na ardhi kiasi cha mkono, mara Kitabu kinamtangulia na kile alichopangiwa, na wakati huo anafanya matendo ya watu wa motoni na akaandikiwa kuwa huo ndio mwisho wake na akaingia motoni; Kwa sababu sharti la kukubaliwa matendo yake ni kudumu katika matendo hayo na wala asibadilishe, na watu wengine wapo wenye kufanya matendo ya watu wa motoni mpaka mtu anakaribia kuingia motoni, mpaka inakuwa kati yake na kuingia motoni ni kiasi cha urefu wa mkono, basi kikamtangulia kitabu na alichopangiwa hivyo akafanya matendo ya watu wa peponi na akaingia peponi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Mwisho wa mambo yote huwa kwa namna ambavyo imekwishapangwa na kukadiriwa.
  2. Tahadhari ya kutodanganyika na muonekano wa matendo; Bali matendo huangaliwa mwisho wake.