+ -

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رضي الله عنهما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ اللهَ سَيُخَلِّصُ رَجُلًا مِنْ أُمَّتِي عَلَى رُءُوسِ الْخَلَائِقِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ، فَيَنْشُرُ عَلَيْهِ تِسْعَةً وَتِسْعِينَ سِجِلًّا، كُلُّ سِجِلٍّ مِثْلُ مَدِّ الْبَصَرِ، ثُمَّ يَقُولُ: أَتُنْكِرُ مِنْ هَذَا شَيْئًا؟ أَظَلَمَكَ كَتَبَتِي الْحَافِظُونَ؟ فَيَقُولُ: لَا يَا رَبِّ، فَيَقُولُ: أَفَلَكَ عُذْرٌ؟ فَيَقُولُ: لَا يَا رَبِّ، فَيَقُولُ: بَلَى إِنَّ لَكَ عِنْدَنَا حَسَنَةً، فَإِنَّهُ لَا ظُلْمَ عَلَيْكَ الْيَوْمَ، فَتُخْرَجُ بِطَاقَةٌ فِيهَا: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، فَيَقُولُ: احْضُرْ وَزْنَكَ، فَيَقُولُ: يَا رَبِّ مَا هَذِهِ الْبِطَاقَةُ مَعَ هَذِهِ السِّجِلَّاتِ؟ فَقَالَ: إِنَّكَ لَا تُظْلَمُ، قَالَ: فَتُوضَعُ السِّجِلَّاتُ فِي كِفَّةٍ، وَالْبِطَاقَةُ فِي كِفَّةٍ، فَطَاشَتِ السِّجِلَّاتُ، وَثَقُلَتِ الْبِطَاقَةُ، فَلَا يَثْقُلُ مَعَ اسْمِ اللهِ شَيْءٌ».

[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2639]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abdullah bin Amrou binil Aaswi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu-Rehema na amani ziwe juu yake-
"Kwa hakika Mwenyezi Mungu atamchagua mtu mmoja katika umma wangu mbele ya mkusanyiko wa watu siku ya Kiyama basi atamkunjulia mafaili tisini na tisa, na kila faili moja lina ukubwa sawa na upeo wa macho yanapoishia kuona, kisha atasema: Je unapingamizi katika haya yaliyopo ndani ya mafaili haya?, je waandishi wangu wenye kuhifadhi yenye kuandikwa wamekudhulumu? basi atajibu: "Hapana ewe Mola wangu, hawakunidhulumu": Basi atamwambia: Je unalakujitetea? Basi atasema: "Hapana ewe Mola wangu", atasema: Hakika wewe unayo matendo mema kwetu, na kwa hakika hautodhulumiwa chochote leo hii, basi atatolewa kadi iliyoandikwa Ash-hadu An-laa Ilaaha illa llaahu wa Ash-hadu Anna Muhammadan Abduhuu wa Rasuuluhu, hivyo atasema: Ewe Mola wangu ni kadi gani hii na ni faili gani hili? Basi atasema: Kwa hakika wewe hutodhulumiwa", Mtume akasema: Basi yatawekwa mafaili katika kipimo na kadi itawekwa upande wapili wa kipimo, basi ukawa mwepesi ule upande uliowekwa mafaili, na ukawa mzito ule upande uliowekwa kadi, na haiwezekani kitu chochote kuwa kizito kuliko neno la Tauhidi ambalo ni Laa Ilaaha illa llaah Muhammadan Rasuulullah."

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2639]

Ufafanuzi

Alitoa habari Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu atamchagua mtu katika umma wake kwenye kundi la watu siku ya Kiyama atamuita ili amuhesabu, basi atamtolea mafaili tisini na tisa na mafaili hayo ni ya matendo yake mabaya ambayo alikuwa akiyafanya Duniani, na urefu wa kila faili ni mfano wa upeo wa macho, Kisha Mwenyezi Mungu atamwambia mtu huyu: Je unapinga chochote katika haya yaliyoandikwa katika mafaili? Je Malaika wangu wenye kuhifadhi wanayoandika wamekudhulumu? Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Je una chochote cha kujitetea nacho katika matendo yako uliyoyatanguliza miongoni mwa matendo ya Duniani?katika matendo uliyoyafanya kwa kusahau au kwa kukosea au kwa kutojua, Basi atasema mtu yule: Hapana ewe Mola wangu sina chochote cha kujitetea nacho. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu atasema: Si hivyo, kwa hakika wewe una mambo yaliyoandikwa kwetu sisi, na kwa hakika wewe hutodhulumiwa leo hii. Akasema: Basi itatolewa kadi iliyoandikwa ndani yake: Ash-hadu An-laa ilaaha illa llaah wa Ash-hadu Anna Muhammadan Ab-duhuu wa Rasuuluhu. Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Angalia Mizani yako. Basi atasema mtu yule hali ya kuona ajabu: Ewe Mola wangu! ni uzito wanini huu wa kikadi kidogo pamoja na kupimwa na mafaili yote haya? Basi atasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: hautadhulumiwa leo hii. Akasema: Basi mafaili yatawekwa katika sehemu ya kupimia, na Kadi kwenye sehemu nyingine ya kupimia; Hivyo basi ukawa mwepesi upande wa kupimia palipo na Mafaili na ukawa mzito upande wa kupimia palipo na Kadi, hivyo basi Mwenyezi Mungu akamsamehe.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Utukufu na ukubwa wa neno la Tauhidi: Kushuhudia kuwa Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu -Laa ilaaha illa llahu-, na uzito wa neo hilo katika Mizani.
  2. Haitoshi kutamka neno tu: Laa ilaaha illa llahu kwa ulimi peke yake, bali ni lazima kujua maana yake na kuyafanyia kazi makusudio yake.
  3. Kuwa na Ikhlaas (kutakasa matendo kwa ajili ya Allah) na nguvu ya kumpwekeha Mwenyezi Mungu ni sababu ya kusamehewa madhambi.
  4. Imani huboreka kwa kuboreka yaliyokuwa moyoni miongoni mwa ikhlas, kwani kuna baadhi ya watu huyasema maneno haya lakini wataadhibiwa kwa kiwango cha madhambi yao.